Unyanyasaji kwa wanawake hasa wanandoa ni suala ambalo limekuwako kwa miaka mingi .Unyanyasaji huu katika namna mbalimbali pia umekuwa wa maneno makali ya kashfa mbele ya watoto au wanafamilia ,kipigo na pengine kifo .Haya yote yana athari kubwa si wanawake wengi wamekuwa wakiugulia kimya kimya machungu haya yanayotokea katika kuta nne za chumba cha ndoa kwa kuogopa aibu,manyanyaso zaidi n.k.
Hata hivyo kwa siku za hivi karibuni wapo wakinamama wenye ujasiri wa kwenda katika vyombo vinavyohusika kutaka msaada.
Kinachosikitisha ni kwamba baadhi ya vyombo hivi vimekuwa vikichukulia suala hili kimzaha mzaha tu.Baadhi ya wahusika wanaliona siyo tatizo kubwa.tunashukuru walau kwa miaka ya karibuni vituo vingi vya polisi vimeanzisha dawati maalum la jinsia.
Tunaomba basi wahusika wayatumie madawati hayo inavyopasa ili suala hili lipungue kama sio kufikia ukomo .Kwa njia hii tunaweza kuwa na hali ya amani na utulivu kwenye jamii yetu na hivyo kuleta maendeleo katika familia.
Ifahamike kuwa baadhi ya familia zinashindwa kusonga mbele kwa sababu kuna ugomvi wa mara kwa mara kiasi kwamba baba na mama wanashindwa kupata nafasi ya kukaa pamoja na kujadiliana kwa ajili ya maendeleo ya familia yao hii ikiwa ni pamoja na masuala yanayohusu watoto..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni