Pages

Jumatano, Machi 20, 2013

HAYA NI MAMBO ANAYOYAPENDA MWANAMKE KWENYE UHUSIANO

Kama mwanamke au mwanaume ni wazi kuwa ukishafahamu siri ya mwenza wako, basi inakuwa rahisi kumpa kile anachohitaji katika uhusiano wenu, Jambo la kwanza ni vyema kufahamu mwanamke na mwanaume ni tofauti yaani kama vile wanatoka sayari tofauti, cha msingi ni vyema kufahamu kuwa mwenza wako hawezi kuwa na tabia kama zako, kwani kila mmoja ana tabia zake, Mambo anayoyapenda mwanamke ni pamoja na kuambiwa neno nakupenda yaani mwanamke yeyote aliye katika uhusiano huwa na hamu ya kusikia  kutoka kinywani kwa mume ama mpenzi wake kwamba nakupenda, neno hili analihitaji mara kwa mara kulisikia masikioni pake haijalishi ni mara ngapi na uwe unamaanisha kutoka moyoni.
kitu kingine mwanamke hupenda mawasiliano na mwenza wake kama kumtumia ujumbe kila wakati, kumpigia simu  huku akimjulia hali au akimtakia siku njema, mchana mwema au kumwambia maneno matamu nk, pia mwanamke hupenda kushirikishwa katika mambo anayoyafanya mwenza wake kwani hujiona kuwa yupo karibu zaidi katika furaha na matatizo ya yule anayempenda.

Jambo la msingi ni kwamba  kama tunataka uhusiano uende vizuri  hatuna budi kujenga utamaduni  wa kusomana tabia zetu ili kufahamu mwenza wako anapenda nini na kitu gani hakipendi,kwani ni wazi kuwa kila mmoja ana tabia zake tofauti.

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Mwanamke hata umfanyie nini hatosheki wala haridhiki...Habari ndo hiyo

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom