ILIPOISHIA
Nilipofika
nyumbani niliwakuta wadogo zangu wakiwa wamekaa nje, Renata ambaye alikuwa
darasa la tatu na Tumaini alikuwa darasa la kwanza. Waliponiona walinikimbilia
huku wanalia “Dada Kandida,, Dada Kandida Baba , baba, baba”Alikuwa akilia
Renata huku akinivuta katika gauni langu nilishindwa kuelewa Baba amepatwa na
kitu gani? “Renata Baba yuko wapi? Mnalia nini? Baba amefanyaje” Nilimuuliza
mdogo wangu wa kike “Baba amechukuliwa na watu, wamempiga Baba”
INAPOENDELEA
Baba amechukuliwa na watu, wamempiga Baba” Alinijibu
kwa sauti yenye kigugumizi, Nilihisi kuchanganyikiwa kwani sikuamini kile alichokuwa anakisema mdogo wangu. Nilikimbia na kuelekea kwa Mama Keku kabla hata sijafika Mama
Keku aliniita “Kandida nipo huku njoo” alikuwa ameketi jikoni kwake akiandaa
chakula. Nilisogea huku nikiwa na shauku la kutaka kujua Baba yangu ameenda wapi?"
Karibu uketi mwanangu, aliongea Mama Keku huku mimi nikiwa namuangalia "Mama Keku Baba yangu amepatwa na kitu gani?" Mama Keku alijaribu kuniliwaza na baadaye akaamua kunieleza hali halisi ya kile kilichotokea.
“Kandida wewe ni msichana mkubwa, fikiria Mama yako na wadogo zako wanakutegemea wewe. Baba yako amepelekwa Polisi” akiwa anaendelea kuongea yale maneno nilihisi kama yananichanganya kichwa changu kabisa. “Ati unasema Baba yangu amepelekwa Polisi, amefanya nini? Baba yangu eeh Mungu balaa gani hili jamani mbona tunateseka hivi” Nijikuta nimekaa chini huku nikilia kwa sauti Mama Keku alijitahidi sana kunibembeleza lakini sikutaka kumsikia.Niliamua kuchukua maamuzi ya haraka na kwenda hadi kituo cha polisi.

“Wewe binti una matatizo gani? Unalia nini?” Ilikuwa
ni sauti ya Askari ambaye nilimkuta pale kwenye mapokezi ya kituo cha polisi
“Namtaka Baba yangu jamani, namtaka Baba yangu” Yule askari akaniuliza “Binti
sasa unavyolia sikuelewi unamtaka Baba yako yuko wapi? ametekwa? au amefanyaje”
Nilikuwa nalia kwa uchungu “Baba yangu amekamatwa na Polisi, na Mama yangu
amelazwa hospitalini sisi tutabaki na nani? Namtaka Baba yangu” Kulikuwa na
askari mwingine kwa pembeni ambaye alikuwa ni mwanamke alinichukua na kuanza
kunibembeleza huku akinisihi ninyamaze na kumuelezea taratibu.
Baadaye walinuliza jina la Baba “Anaitwa Kitali Shirima” Askari mmoja akacheka “Hahahaha huyo mzee aliyeletwa hapa kwa kosa la kuiba pesa kutoka katika kiwanda cha plastiki” Nilimuangalia Yule askari na kumwambia “Baba yangu siyo mwizi jamani hawezi kufanya hivyo” Nilihisi kama sielewi kabisa kile nilichoambiwa eti Baba yangu mwizi? Hapana haikuniingia akilini. Niliomba niende kumuona "Subiri hapo Baba yako akaitwe atakuambia ameiba nini?"

Baba aliitwa, kwa namna alivyokuwa anaonekana alikuwa
amechoka na huku akionekana kuwa na majeraha mikononi na kwenye paji la uso
wake. Machozi yalinitoka huku nikimuangalia kwa uso uliokosa amani. Baba alinisihi nirudi
nyumbani na nisimwambie Mama chochote kuhusu hali yake. “Mwanangu wewe nenda
nyumbani mimi nitakuwa salama, nitatoka siku yoyote usijali. Nenda ukawaangalie
vizuri wadogo zako pamoja na Mama yako usimwambie chochote kuhusu mimi." Muda wa
mazungumzo uliisha na Baba alirudishwa katika chumba cha Mahabusu.
Niliondoka na kuelekea nyumbani nafsi yangu ilikuwa
inaumia sana “Chanzo ni umasikini , Baba yupo gerezani kwasababu ameiba pesa
kwaajili ya matibabu ya Mama, lakini kwanini aliiba jamani,kwani ametenda kosa na sasa hakuna mtu wa kutusaidia, sasa sijui hata
nifanyeje nani atanisaidia mimi” Niliongea na nafsi yangu huku nikiwa nimepoteza
matumaini. Nilipofika nyumbani Mama Keku alinipa matumaini kuwa nisikate tamaa
Mungu atatusaidia Mama atapona na Baba atatoka gerezani. Niliingia jikoni na
kundaa chakula kwaajili ya wadogo zangu na baadaye nilirudi hospitalini
kumwangalia Mama.
Tayari Mama alikuwa amefanyiwa upasuaji, na kwa muda nilioenda alikuwa amepumzika nilibaki pale hospitalini mpaka asubuhi. Ambapo baadaye Mama alizinduka na kwa wakati huo alikuwa akihisi maumivu kutokana na kidonda cha upasuaji na nyuzi alizoshonwa ndiyo zilikuwa zinampa maumivu makali. Daktari alinisihi nisiwe na waswasi hali ya Mama itatengamaa.
Baada ya wiki mbili tokea Mama afanyiwe upasuaji hali yake ilianza kutengamaa hivyo aliruhusiwa kurudi nyumbani, kwa wakati wote huo Mama alipokuwa akiniuliza kuhusu Baba nilimwambia Baba amesafiri.Lakini aliporudi nyumbani ilimchukua siku chache akafahamu ukweli kuwa Baba alikuwa amekamatwa na Polisi “Masikini mume wangu chanzo ni mimi,Mungu tusaidie” Mama alihuzunika sana baada ya kufahamu kilichomtokea Baba ambapo kwa wakati huo Baba alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.

Maisha yaliendela hali ya Mama ilikuwa ni njema aliweza
kuandaa chakula na kumpelekea Baba gerezani mara kwa mara. Kwa upande wangu
nilikuwa nimekaa nyumbani kwa kipindi kirefu bila kwenda shule.Kutokana na
hali ya pale nyumbani Mama aliniambia
hawezi kunilipia ada ya shule kwahiyo ilinibidi nibaki nyumbani ,
ijapokuwa nilitamani sana kusoma lakini kutokana na hali halisi ya maisha ya
pale nyumbani sikuwa na namna nyingine yoyote.Nini kitaendelea usikose sura ya ......5..........
Maoni 2 :
Dah inasikitisha sana
Kisa muruwa tupo pamoja mpendwa
Chapisha Maoni