Jumanne, Mei 14, 2013

ANAOMBA USHAURI "Mume wangu hataki nifanye kazi wala kujiendeleza kielimu na mimi natamani kusoma"

Habari yako Adela mimi ni mwanamke, mwenye umri wa miaka 27. nimeishia kidato cha nne. Lakini sikuweza kufanikiwa kufanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne.Nimeolewa mwaka 2006, na kufanikiwa kupata mtoto ambaye kwa sasa ana umri wa miaka mitano.Tatizo langu ni kwamba natamani sana kujiendeleza kielimu lakini mume wangu anakataa. Au nikitaka kufanya kazi yoyote mume wangu hataki .Na mimi sipendi kuwa tegemezi maana kuna wakati natamani kurudi kwetu ili niweze kuendelea na masomo.Maana najua hata ningekuwa na hela  yangu binafsi ningesoma QT na yeye asingejua kwani ni mtu wa kusafiri angestukia tu nimemaliza sasa sijui nifanyeje ili mume wangu anielewe natamani sana kurudi shule naombeni ushauri

Maoni 6 :

Unknown alisema ...

Pole sn dada!! ila endelea kumshawishi mume wako inawezekana siku moja akakuelewa na kulikubali ombi lako,maana maisha haya ni kusaidizana sababu kuna leo na kesho!Lakini pia utakapopata hiyo fursa ujitahidi uitumie vizuri, mume wako hawezi kukataa tu hivihivi lazima na yeye ana sababu zake tena za msingi.Ila jitahidi kumuelewesha na atakuelewa tu!!

Bila jina alisema ...

ndugu yangu huyo mume wako anahitaji ushauri wa wazazi aache mambo ya kizamani akuruhusu ufanye kazi

Bila jina alisema ...

ndugu yangu huyo mume wako anahitaji ushauri wa wazazi aache mambo ya kizamani akuruhusu ufanye kazi

Bila jina alisema ...

POLE SANA NDUGU ENDELEA KUMBEMBELEZA USIFANYE SIRI KWANI AKIGUNDUA ITAKUWA BALAA.

Bila jina alisema ...

Mbembelezee kitandani wakati unampa yale mambo matamu.Mwambie mume wangu nakushukuru sana kwa jinsi unavyonijali na kunithamini hasa kwa kunipa mapenzi matamu sana,kweli unanifanya nijisikie mwanamke na nifurahie sana kupata mwanaume kama wewe.Halafu chomekea hilo ombi lako taratibu kuwa mume wangu yaani nakushukuru kila wakati ukiwa mbali natamani ufike haraka,yaani ni sawa na vile ninavyotamani kuongeza elimu kwenye maisha yangu maana inaweza pia kuniongezea ujasiri, ufundi, uelewa, ufahamu wa jinsi ya kuishi na kupambanua mambo mengi yanayotuzunguka na kuniwezesha kuwa mama bora wa familia yetu na mke bora wa... taja jina lake hapo.Mengine mengi utaongezea hapo mimi nimekufungulia utangulizi tu.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom