Kuna baadhi ya wanaume na wanawake ambao huwa na tabia ya kuhukumu bila ya kuuliza. Pale inapotokea jambo fulani mfano inapotokea mvulana na msichana wanapozoeana basi watu wa pembeni au wao wenyewe yawezekana mmoja akapakazia mambo ambayo ni kinyume na urafiki wao. Yaani atatia chumvi na kufanya watu wahisi kuwa ni wapenzi kumbe sivyo. Lakini pia akionekana mwanamke na mwanaume wakiwa pamoja mara kwa mara baadhi yao moja kwa moja husema ni wapenzi na hata kudiri kupeleka maneno kwa mume ama mke wa yule aliyemuona bila ya kuwa na uhakika. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni