Pages

Jumatatu, Mei 27, 2013

SIMULIZI......BADO MIMI ..SURA YA ......16....... ILIPOISHIA
Machozi yalinibubujika nguvu ziliniishia nikajikuta nimekaa chini huku nikijikunyata kama mtu anayehisi baridi kali nililia sana "Eeeh Mungu nisaidie nitoke eneo hili, Masikini Baba yangu yalaiti ningelijua kuwa Mama  Bilionea ni mtumwa wa Shetani, yote haya yasingenikuta mimi pamoja na familia yangu.Mateso gani haya jamani, sijui nini hatima ya maisha yangu." Je.....NINI KITAENDELEA USIKOSE ....SURA YA 16.........

 INAPOENDELEA
Kwa wakati wote huo nilikuwa nahisi kama nipo ndotoni lakini haikuwa ndoto, niliumia sana moyoni kumuona Baba yangu katika hali aliyokuwa nayo. Alikuwa amevaa nguo zimechanika huku nywele zake zikiwa ndefu bila ya kupitishwa kitana.Uso wake ulikuwa umepoteza nuru ya maisha nilikuwa nikimtizama anapoelekea lakini baadaye sikumuona tena. Moyoni mwangu niliwaza "Eeeh Mungu nakuomba unisaide, Mama Bilionea anataka kuiangamiza familia yangu ili aje kutufanya misukule. 

Nawezaje kutoroka eneo hili? Nataka nikamuokoe Mama yangu jamani". Nikiwa nawaza Chande alinisemesha "Kandida nimekuambia huu ni muda wa kwenda kula unaweza kujumuika pamoja na mimi lakini sikuelewi, sizani kama upo sahihi kutoa machozi eneo hili. Kwani hapa watu huwa hawalii unaweza kupatwa na chochote kibaya. Na ikiwezekana unaweza  usitoke kabisa eneo hili maisha yako yote ukaishi  katika hekalu la Bibi Bilionea". 

Nilinyanyuka pale chini huku nikiwa najifuta machozi yaliyokuwa yakibubujika katika paji la uso wangu na kusema "Chande naomba unisaidie niondoke katika hili hekalu,siwezi kubaki huku" Chande alinitizama kwa kunikazia macho "Nimekuambia huu ni muda wa kwenda kula, na pia kuhusu kuondoka katika hili hekalu ni mpaka utakapoonana na Bibi Bilionea"Aliongea kwa sauti kali kuonyesha msisitizo. Tuliongozana hadi katika eneo ambalo watu wote walikuwa wameketi huku wakila chakula ambacho kilikuwa ni pumba pamoja na damu ambayo sikujua wameipata wapi damu ya binadamu. nilishindwa kuamini ninanchokiona mbele yangu kwani zile pumba zilikuwa zimemwagwa chini na huku kila mmoja akiwa ameshikilia kikombe cha ajabu kilichokuwa na damu "Natamani hii ingekuwa ni ndoto jamani, haya ninanyoyaona yanatisha sana" .


Nilikuwa natizama huku na kule  wakati huu nilimuona tena Baba yangu naye akiwa anakula pumba huku akinywa damu nilimtizama huku nikiwa nasikitika, Kutokana na nilivyokuwa nikimtizama kila mara, alinyanyuka pale alipukuwa ameketi na kunifuata. wakati akiwa anakuja nilihisi labda atakuwa  amenikumbuka, Alikuja kwa kasi ya ajabu na kunishika shingoni kwa mikono miwili huku akilia  kwa sauti ya ajabu alikuwa akininyonga na kutaka kunidhuru. "Mamaa, nimmm, nakufaaaa." Nililia kwa sauti lakini  hakuna aliyekuwa akinitizama wala kunisaidia. Nilijaribu kujitoa kwenye mikono ya Baba bila mafanikio kwa Bahati nzuri Chande alitokea na kunisaidia. Baba aliondoka huku Chande akimpa ishara ya kwamba aendelee kula chakula chake.

Huku nikiwa natetemeka na kukohoa kana kwamba kuna kitu nimemeza kikanikaba kooni. Nilikuwa najisikia maumivu makali eneo la kwenye shingo kama si Chande Baba angeniuwa. Chande alinitizama na kusema "Nilikuambia kaa mbali  na huyu Mzee, siyo binadamu unayemfikiria huyu tayari ni mtu mwingine atakudhuru. Inamaana tunashindwa kuelewana Kandida?" Aliongea huku akionekana kuwa na hasira na jazba "Naomba unisamehe Chande nisaidie, nipeleke kwa Bibi Bilionea siwezi kubaki huku nisaidie Chande" Niliendelea kumbembeleza sana ili anipeleke lakini alinisihi kuwa haikuwa siku nzuri kwa mimi kwenda kumuona Bibi Bilionea.

Nishinda siku hiyo Bila kula chochote na huku nikiwaza nini hatima ya maisha yangu. Nilimfuata Chande kila alipokuwa akienda kwani kwa wakati huo nilikuwa nimeshajua kila aliyenizunguka anaweza akanidhuru.Katika lile eneo ilikuwa ni vigumu kufahamu muda wala siku husika. Kutokana na uchovu mwingi nilijikuta usingizi umenipitia huku nikiwa nimeketi chini ya mti pamoja na Chande. Baadaye Chande aliniamsha "Kandida, Kandida, sikiliza kwa umakini huu ni muda mzuri wa kwenda kuonana na Bibi Bilionea".

 Nilishtuka kutoka usingizini kulikuwa na giza nene yaani nilikuwa sioni chochote  lakini macho ya Chande yalikuwa yanan'gaa kama tochi yenye mwanga mkali sana. Niliogopa nakusema "Chande ni wewe! Mbona sioni kitu na macho yako ....yana..." Chande alinikatisha nisiendelee kuongea"Shiiiii, usiongee kwa sauti kubwa, wakubwa watakusikia. Hatuna muda wa kupoteza twende haraka" Alikuwa akininon'goneza kwa sauti ya chini sana nilinyanyuka taratibu na kumfuata huku yeye akiwa ananiongoza kwa kumulika njia na macho yake. Muda wote nilikuwa nahisi baridi kali sana na pia sikuona chochote zaidi ya mwanga wa macho ya Chande. Tulitembea mwendo mrefu wa takribani kama nusu saa. 

Kwa Mbali niliona mwanga mkali sana Huku kukiwa na mti mrefu sana ambao matawi yake yalionekana  kun'gaa sana"Unapaona pale ndiyo kwa Bibi Bilionea sasa tukifika usiongee chochote kwani tayari anajua kuwa tunaenda kwake.Unachotakiwa kufanya  nikumsikiliza atakachokueleza. Atakapokuuliza swali uwe na majibu mazuri. Hii ndiyo nafasi yako yakurudi duniani" Nilikuwa naogopa sana lakini nilijipa moyo na ujasiri kwani nia yangu nilikuwa nataka nirudi kwa Mama yangu na wadogo zangu. JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SURA YA.......17.....ambayo itaendelea siku ya Alhamisi. KESHO USIKOSE KUFUATILIA SIMULIZI YA.... HAKUNA SIRI.....

Maoni 2 :

kavishe alisema ...

interesting...

Bila jina alisema ...

Mhhhhhh makubwa hya!nasubr kwa hamu.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom