ILIPOISHIA
Baadaye Mama
Robert alijiandaa na kwenda kumpokea mume wake ilikuwa ni furaha isiyo na
kifani, Mama Robert alimkaribisha mume wake pamoja na watoto wake kwa furaha na
baadaye walielekea nyumbani. Ambapo moja kwa moja walienda kukoga kwanza na
baadaye walienda mezani kupata chakula cha jioni. Wakati huo Joyce
alikuwa amejipumzisha chumbani kwake kwa
muda mrefu hivyo hakuonana na wageni.NINI KITAENDELEA USIKOSE ....SURA YA....10
INAPOENDELEA
Baadaye Mama Robert aliamua kumuita Joyce ili amtambulishe kwa mume
na watoto wake “Joyce mwanangu” aliita Mama Robert Joyce akiwa chumbani
aliitika huku akinyanyuka na kuelekea sebuleni “Abee mama” Alipofika kwa
mshangao Yule baba alikuwa kama amemfananisha Joyce kisha akauliza “Huyu binti
ni nani mama Robert?” Aliuliza lakini kabla hajajibiwa Joyce aliwakatisha
kwa kumsalimia “Shikamoo Baba” Aliitika “Marahaba” Mama Robert akaanza
kumtambulisha, "Mume wangu huyu binti anaitwa Joyce ni msichana wa kazi
hapa nyumbani ni binti mpole na anajua sana kufanya kazi” Baba Robert akasema
“Alaa karibu sana binti karibu uketi” Joyce alijisogeza taratibu na kujumuika
pamoja nao.
Baba Robert aliendelea na maswali “ Joyce wewe umetokea
wapi? na wazazi wako wanaishi wapi”? Joyce akamjibu mimi nilikuwa nikiishi
hapahapa Dar es salaam, sina wazazi kwani walishafariki” alisema Joyce kwa
sauti ya upole. “Pole sana binti baba yako alikuwa anaitwa nani na inamaana
hauna ndugu”? Aliuliza maswali mengi kwa wakati mmoja. Joyce alimjibu na kusema
“ Baba yangu alikuwa anaitwa Ndesanjo Kimaro, kuhusu ndugu sikuwahi......” Kabla
hajamalizia kuzungumza Baba Robert alimkatisha "Unasema Ndesanjo Kimaro?”
Wewe ni mtoto wa Ndesanjo alikuwa anafanya biashara ya bidhaa za kilimo” Joyce
alishangaa kuona Baba Robert anamfahamu baba yake kwani ni kweli baba yake
alikuwa akijishughulisha na biashara ya bidhaa za kilimo, akasema “Ndiyo baba
yangu alikuwa anafanya biashara hiyo”
"Mungu wangu kumbe Ndesanjo alifariki Mama Robert huyu mtoto ni
ndugu yangu kabisa. Ndesanjo ni mdogo wangu tumezaliwa na Baba mmoja lakini
hatukuwasiliana ni muda mrefu tokea nilipokuwa nje ya nchi kikazi. Siamini
ninachokisikia, lakini pia si alikuwa na watoto wawili na mwingine wa kiume,
yuko wapi mdogo wako?” Joyce aliinama chini kwa uchungu huku machozi
yakimtoka akasema “Baba na Mama walifariki kwa ajali ya gari, na Mdogo wangu
amefariki alikuwa anaumwa sikuwa na pesa za kumpeleka Hospitali” Baba Robert
alihuzunika sana baada ya Joyce kumsimulia kila kitu, aliahidi kumsaidia Joyce
katika maisha yake yote.
Maisha ya Joyce yalibadilika sasa alikutana na ndugu zake aliishi kwa
furaha na walimpenda sana. Kuna wakati Joyce alikuwa akiwaza “Yalaiti mdogo
wangu angelikuwa hai. Tungeishi pamoja haya maisha ya furaha” Siku zilienda
baadaye Yule baba yake mkubwa aliamua kumpatia kazi Joyce katika
duka lake la vifaa vya ujenzi na kumlipa mshahara kila mwisho wa mwezi.
Maisha yaliendelea Joyce alipendeza sana. Kwani alikuwa ni msichana
mrembo ambaye kila mwanamume aliyekuwa akimuona alivutiwa naye, Joyce
alifahamiana na watu mbalimbali na wengi walikuwa wakikutana pale dukani. Ilipita
miaka miwili tokea maisha ya Joyce yabadilike na alisahau matatizo aliyokutana
nayo kipindi cha nyuma. Ilifikia kipindi akapata rafiki ambaye alikuwa
anaitwa Fredy, walikuwa ni marafiki sana.Baadaye walifikia hatua ya kuwa
wapenzi.
Siku moja Fredy alimfuata Joyce dukani ilikuwa ni jioni mida
ambayo Joyce alikuwa akifunga duka “Habari mpenzi naomba leo tutoke kuna
kitu cha muhimu nataka tuongee” Joyce alimjibu akisema “Mmmh Fredy kitu
gani hicho mpenzi leo sitaki kuchelewa kurudi nyumbani si unajua Baba na mama
ni wakali hawapendi nichelewe” “Hapana yaani haitachukua muda mrefu
nitakurudisha mapema” Alisema Fredi “Basi hakuna tatizo ngoja nimalizie kazi
haraka, nifunge duka tuondoke” Fredy aliondoka na kwenda kumsubiriJoyce katika
gari lake aina ya Rav 4.
Baadaye Joyce alimaliza kazi zake na Kumfuata mpenzi wake kisha
waliondoka na kuelekea maeneo ya Posta, Walitafuta sehemu tulivu maeneo
ya City Garden kwa ajili ya mazungumzo walikaa pale huku
wakiendelea kupata vinywaji Fredy alianza kwa kusema “Joyce mpenzi unajua
tumekuwa katika mahusiano kwa muda mrefu natamani sasa uwe mama wa watoto wangu,
nadhani sasa ni wakati mzuri tufunge pingu za maisha.” Alisema Fredy,
Joyce aliyekuwa anakunywa Juisi kwa wakati huo
alishusha glasi yake mezani. Kisha alimkumbatia mpenzi wake kwa furaha “
Jamani Fredy nimefurahi kusikia hivyo, nami nakupenda sana nipo tayari maisha
yangu niishi na wewe katika shida na raha
nakupenda sana mpenzi” Basi ilikuwa ni
furaha, waliendelea kuzungumza na baadaye waliondoka. Fredy alimrudisha Joyce
nyumbani kwao wakiwa njiani Fredy alitoa ahadi ya kwenda kujitambulisha rasmi
kwa kina Joyce mapema siku za usoni. JE NINI KITAENDELEA......USIKOSE SURA YA......11
Maoni 2 :
Daaaah! kweli hakuna marefu yasiyokuwa na ncha pia ukipata majaribu ukavumilia lazima ushinde tu. afadhali mungu kamkumbuka joyce kafanikiwa kukutana na ndugu yake. mola awe naye cku zote za maisha yake
kwann hanafanya haraka joyce jmn?badala ya kilio ss furaha bora.
Chapisha Maoni