Pages

Jumatano, Julai 03, 2013

MANENO MAZURI KWA YULE UMPENDAYEKwa kawaida busu la mafanikio hubusiwa usoni, busu la amani hubusiwa mashavuni, busu la upendo hubusiwa mdomoni, busu la mapenzi hubusiwa shingoni.Je wapi nikubusu, ili ulale kwa raha mpenzi.
******************************************************
Hakika mtoto umeumbika mithili ya malaika, japo Mbinguni, sijafika lakini na uhakika kwa kila mwanaume aliyekamilika akikuona lazima atatamani kuwa na wewe, naomba japo  yako dakika nipate kukueleza yaliyonifika moyoni, kwani siwezi tena kukuficha jinsi ninavyokupenda. nakupenda amini kwako  nimefika.
*****************************************************
Mapenzi si pombe lakini yanalewesha,wala si dawa, lakini yanaua, wala si kifo lakini yanaliza, wala si katuni lakini yanafurahisha wala si fimbo lakini yanaumiza.Ni mimi tu mwenye mapenzi ya kweli  kwako, nipende daima mpenzi.

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Daaaaaah,! maneno mazuri na matamu kweli kweli. big up dada adela kwa maneno hayo na 2naomba u2pe maneno mengine matamu

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom