Jumapili, Septemba 22, 2013

HONGERA HAPPINESS WATIMANYWA KWA KUNYAKUA TAJI LA MISS TANZANIA 2013 KILA LA HERI.

Happiness Watimanywa, msichana pekee kutoka Tanzania aliyeweka historia ya kuongoza nchi zaidi ya 150 za mtandao wa IGCSE katika somo la Uhasibu kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka 2010.

Happy (19) ni mzaliwa wa familia ya kawaida sana ya Mr Louis Roussos ya Morogoro. Wadogo zake Angel na Romeo sasa wanasoma St. Constantine shule iliyomtoa Happy. Pia, Happiness Watimanywa amewahi kusoma Laureatte International School ya Dar-es-salaam, ambapo akiwa hapo, alikutana na mwalimu wa michezo Mr Tchalewa Ndeki ambaye alimfungulia mipaka mingi Happy. Akiwa Laureatte, Happy aliwahi kwenda China na South Korea akiwa na wanafunzi wenzake katika matamasha mbali mbali ya elimu na michezo. Baada ya kumaliza kidato cha nne, Happy alifanikiwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Strathclyde cha UK ambapo anasomea digrii ya Biashara.
HONGERA SANA MREMBO KILA LA HERI

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom