Siku moja akiwa jijini Dar es salaam katika shughuli zake alikutana na dada mmoja ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa chuo na walifahamiana, na kisha kubadilishana namba za simu. Baadaye waliendelea na mawasiliano wakiwa kama marafiki na hatimaye baadaye Jerome aliamua kufungua ukurasa wa mapenzi katika moyo wake na sasa alimpenda sana binti huyu aliyejulikana kwa jina la Selina makazi yake yalikuwa ni Dar es salaam, mara nyingi Jerome alikuwa akija Da es salaam na wakati mwingine huyu mchumba wake alikuwa akienda Dodoma mapenzi yalikuwa motomoto. Jerome aliamini kabisa kuwa Selina angekuja kuwa mke wake alijitolea kwa kila kitu yaani aliamua kumlipia ada ya chuo na matumizi mengine.
Baada ya mwaka mmoja, Selina akiwa ndiyo anamaliza masomo yake ya chuo, Jerome aliamua kumwambia kuwa wafunge pingu za maisha pindi atakapomaliza chuo. Jambo ambalo Selina alimuhakikishia kuwa asiwe na shaka kwani wangefunga ndoa.
Jambo la kushangaza baada tu ya Selina kumaliza chuo ikiwa ni miezi michache imepita, siku hiyo Jerome alikuwa amempigia simu, mwanzoni simu hiyo iliita bila kupokelewa na baadaye ilipokelewa na sauti iliyosikika ilikuwa ni ya mwanaume "Habari yako samahani naomba kuongea na mwenye simu" Alisema Jerome "Wewe nani, unapiga simu usiku, na kusumbua watu wakiwa wamelala, ehee ulikuwa na shida gani? mwenye simu amelala, mimi ni mume wake unaweza kusema ulikuwa na shida gani?"
Jerome hakuamini kile alichokisikia aliona kama ni ndoto alibaki ameduwaa na yule kaka alikata simu. Kesho yake Jerome hakufanya kazi kabisa alikuwa na mawazo sana, akaamua kufunga safari hadi Dar es salaam, alipofika alienda moja kwa moja hadi kwa ndugu zake na Selina na ndipo alipoambiwa ukweli kuwa Selina ameolewa siku za karibuni. Jerome aliumia sana moyoni huku akiwa haamini kilichotokea katika maisha yake. Jerome alikuwa si mtumiaji wa pombe lakini tokea hapo aliamua rasmi kuanza kuwa mlevi ili aweze kupoteza mawazo na pia alijikuta akijiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na wanawake tofauti tofauti, kila kukicha na sasa biashara zake zilikuwa haziendi vizuri kama mwanzo.
Baadaye Jerome alikuja kuugua sana na alipoenda kupima aligundulika kuwa ameathirika na virusi vya UKIMWI. Alilia sana na kujuta yote aliyokuwa akiyafanya "Eeeh Mungu naomba unisamehe, sikujua kama mapenzi yangeweza kuyaharibu maisha yangu kiasi hiki, nawashauri watu wote hasira ni hasara, unaweza kufikiri kunywa pombe au kuwa na wanawake tofauti tofauti, vinaweza kutuliza maumivu katika mapenzi, fahamu kuwa unajidanganya mwisho wake ni mbaya sana. ama kweli POMBE SI DAWA YA MAPENZI maumivu yaliyopo moyoni mwangu yamebaki palepale.
Maoni 4 :
Ninapenda sana hii stori. Kazana mama kutunza utamaduni wetu kupitia simulizi zako zenye mafunddisho mazuri yanayoendana na mila na desturi za watanzania.
Naweza nami kupata bloger yangu?
Jamaniii inaskititisha kwa Jerome...pole sana
Kwakweli Jerome pole Sana na Mimi nateseka ivyoivyo ILA nimetulia nimtafute anaye nipenda kwa zati
Chapisha Maoni