Jumapili, Oktoba 06, 2013

BABA ANAPOKIMBIA MAJUKUMU YA KUMLEA MTOTO, DAMU YAKE.

Inatokea katika maisha, baadhi ya kina dada anapopata  ujauzito na baba wa mtoto kukimbia majukumu ya kulea mtoto,  na wengine kudiriki kusema  kuwa mtoto si wa kwake lakini ikitokea baadaye mtoto amekuwa ndiyo Baba anajitokeza  na kutaka kujitambulisha kama Baba wa mtoto.

 Kuna dada mmoja  anaitwa Lina anasema "Mimi nimepata ujazito kabla ya ndoa lakini sikuona kama ni tatizo kwani nina uwezo wa kumlea mwanangu kutokana na kazi niliyonayo, lakini cha ajabu huyu mchumba wangu nilipomuambia kuwa nina ujauzito amekataa na kusema mtoto si wa kwake, na kisa ni kwamba anataka kuoa hivi karibuni. Imeniuma sana kwasababu kwa asilimia mia moja ujauzito nilionao ni wa kwake. Sasa ninachokiwaza ni kumlea mwanangu peke yangu na hapo baadaye sitaki kabisa aje kurudi na kumtaka mtoto wake nitamfukuza kabisa nimemchukia na sitaki hata mwanangu aje kumtambua kama Baba yake." 

Kwa kiasi kikubwa hasira ndiyo zinapelekea kutokea kwa hali hii wengine huamua kutoa mimba ama kumtelekeza mtoto baada ya kujifungua. Jamani kina Baba msikimbie majukumu ya kulea mtoto, na kina Mama ni vyema kuwa wavumilivu inapotokea hali hii, kinachotakiwa ni kupambana ili uweze kumlea mtoto wako katika mazingira mazuri.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom