Pages

Ijumaa, Februari 21, 2014

UJUMBE WA LEO "Wakati mwingine wanaokataa kukusaidia wanakupa nafasi ya kufanikiwa zaidi"

Miaka minne iliyopita, Brian Acton alipeleka maombi ya kazi katika kampuni kubwa za mitandao ya kijamii za Facebook na Twitter. Kampuni zote mbili zilikataa kumpa ajira akarudi mtaani. Lakini hakukata tamaa, akashirikiana na marafiki zake kuanzisha kampuni ya WhatsApp na ikafanikiwa. Leo, mwaka 2014 kampuni ya Facebook inainunua kampuni ya WhatsApp kwa dola za Kimarekani bilioni 19. Kuna wakati tunakosa nafasi tunazoona ndizo mkombozi wa maisha yetu, badala ya kutumia muda mwingi kuangalia tulipokosa na kujilaumu ni bora kuangalia mbele na kuweka bidii zaidi, uvumilivu na kujituma. Wakati mwingine wanaokataa kukusaidia wanakupa nafasi ya kufanikiwa zaidi. Hapana inaweza kuwa baraka. NA MWAMVITA MAKAMBA

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom