Katika maisha unaambiwa ni vyema kujipenda wewe mwenyewe kabla haujapendwa, kwani kama wewe mwenyewe hujipendi ni vigumu kumpata mtu ambaye atakupenda kwa moyo wake wote, Kitu kingine wanasaikolojia wanakuambia "Kuonyesha penzi lako lote mapema kwa yule umpendaye ni kosa kubwa, Unachotakiwa kufanya ni kumfanyia utafiti anayekupenda ili kumjua undani wake na hiyo itakuwa njia ya kwanza, Ikifuatiwa na kumpa penzi mtu uliyempenda hatua kwa hatua baada ya kupata jibu kuwa ni mkweli. Kumbuka mapenzi yanaumiza sana usipokuwa makini. Inawezekana mtu akawa anakupa kila kitu unachohitaji lakini akawa si mkweli katika mapenzi, kwani unaambiwa mtu kukupa kila kitu si kwamba anakupenda kwa dhati wakati mwingine ni giliba tu. Mapenzi ni utu na siyo kitu.
Wapo baadhi wanaopewa magari,majumba lakini hawana raha nazo. Kumbuka mapenzi kwanza hivyo vitu vingine viwe ni vya ziada kinachohitajika ni mapenzi ya dhati, lakini pia ni vyema kumshirikisha Mungu pale unapotaka kuanziasha uhusiano. Kwani maumivu ya mapenzi hayapo kwa wale wenye uwezo kifedha pekee, hata wenye maisha ya kawaida, Unaweza ukampata mtu ukampenda kwa moyo wako wote, ukamuheshimu kwa kila jambo, na kuvumilia maisha ya shida mliyonayo, lakini kama hakuna mapenzi ya kweli lazima maumivu yatokee, chanzo kikubwa ikiwa ni kukosa uaminifu.
NI VYEMA KUCHUNGUZA KABLA YA KUPENDA, NA PIA KUMBUKA KUJIPENDA MWENYEWE KABLA HAUJAPENDWA.......Unapompenda mtu kiasi kwamba unashindwa kula, kufanya kazi au kufikia hatua ya kutaka kujiua kwasababu ya mapenzi hiyo ni hatari sana unatakiwa kukumbuka kabla ya huyo mtu si ulikuwa unaishi vizuri na maisha yalikuwa yanaendelea sasa kwanini umpende mtu kiasi kwamba ufikie hatua ya kushindwa kuishi bila yeye, huku ukiwa unaambulia maumivu tu badala ya mapenzi.USIKUBALI KUWA MTUMWA WA MAPENZI. MPENDE AKUPENDAYE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni