Jumatatu, Machi 24, 2014

Embu soma mkasa huu "Kidole changu kimeoza na kukatwa baada ya kupaka rangi ya kucha isiyo sahihi'


Kuwa makini na matumizi ya rangi ya kucha kwani inawezekana ukapata madhara, kwa kupaka rangi ya kucha ambayo ni feki.Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Sarah Greenaway (17), amekatwa kidole chake baada ya kuanza kuoza kutokana na kupaka rangi ya kucha isiyo sahihi, Msichana huyu alifikia maamuzi ya kuwataarifu madaktari wamkate kidole chake baada ya kuona kinaanza kuoza. Sarah Greenway alijikuta  akiugulia maumivu makali huku akiwa ameathiriwa na maambukizi ya kuoza, baada ya kupaka rangi hiyo ya kucha aliyoinunua kwa paundi 3.20.

Msichana huyo ambaye ni mfanyakazi wa bar amesema kidole chake kilikuwa kimegeuka na kuwa rangi nyeusi na kwamba alipoona dawa za kuzuia kidole hicho kisiharibike zimeshindwa alikimbizwa hospitali kwaajili ya kufanyiwa upasuaji wa kuondolewa kidole kwani alikuwa katika maumivu makali.Kutokana na hali hiyo madaktari hao waliona vyema kukata kidole hicho kidogo cha mwisho katika mkono wa kulia. Taarifa zaidi zinadai kuwa  kutokana na matumizi ya rangi hiyo ya kupaka kucha isiyo sahihi, ilimsababishia maambukizi ya MRSA, na kufanya kidole kioze na kisha kukatwa katika Hospitali ya Royal Gwent Hspital mjini Newport nchini Uingereza. 

Kutokana na hali hiyo inadaiwa kuwa Sarah kwasasa anaendelea  kupata matibabu ya kuponya jeraha lake  na kwamba anafikiria kuchukua hatua za kisheria. Amesema "Vyote hivi nimevipata kwa sababu ya kucha zangu ili nionekane mzuri.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom