Pages

Jumamosi, Machi 22, 2014

MADHARA YA KUTIZAMA TV, NA KUTUMIA KOMPYUTA KWA MUDA MREFU.


Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia Denis Munga amesema "Tatizo baya ambalo halijafahamika sana na wazazi  ni lile la upungufu wa uwezo wa akili wa watoto, kutokufanya kazi kwa ufasaha ni lile la kuangalia sana TV na kuchezea kompyuta kwa muda mrefu. Muda mwingi wanaotumia watoto katika kuangalia TV na kutumia Kompyuta ni hatari kwasababu kitendo cha kufanya hivyo kwa muda mwingi kinachosha ubongo na kusababisha mwili kuchoka  na ubongo wenyewe kupoteza uwezo wake wa kutafakari mambo kwa kina. Na hili si kwa watoto tu, bali hata kwa watu wazima".

Kisaikolojia anasema, ubongo hautakiwi, kushughulishwa na kompyuta kwa muda zaidi ya saa mbili mfululizo, hata kama kazi anayoifanya mtu ni ile ya kuchati kwenye facebook. Kukosa muda wa kupumzisha akili na kuendelea kufanya kazi za kompyuta kwa muda mrefu na kuangalia TV kwa muda mwingine wa saa 4 mpaka 5 kwa siku, akili ya mtu mwenye kufanya hivi huchoka zaidi na kupunguza uwezo wake wa kufanya kazi. Ameshauri ni muhimu kufanya mazoezi ya viungo "Unapofanya mazoezi ya mwili unasababisha mwili kuwa katika hali nzuri na akili nayo kufunguka na kutafakari mambo kwa kina.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom