Jumanne, Machi 25, 2014

Wanafunzi "Simu ya mkononi inatusaidia kwasababu ya shughuli za masomo" Wadau wasema "Haziwasaidii, zinawapotosha"


Siyo sahihi wanafunzi kwenda shuleni wakiwa na simu, kwani utafiti unaonyesha, mitandao ya simu ya internet inachangia kuwaharibu wanafunzi hususani wa sekondari kuanzia na shule za msingi, hivyo kuwaruhusu waende shuleni na simu ni sawa na kutoa ruhusa ya kuwaingiza kwenye matatizo.

Mbona miaka ya nyuma simu hazikuwepo lakini wanafunzi walikuwa wanasoma vizuri tu, lakini leo wakati huu wa utandawazi ndiyo mambo yamekuwa  mabaya kabisa kwenye elimu. Wanafunzi wanamiliki simu ambazo wao na wazazi wao wanadhani kuwa zinasaidia  lakini wanafanya vibaya kwenye mitihani, hivyo ni vyema wale wanaotaka kwenda na simu shuleni wakajua kuwa ni hatari kwa mustakabali wao na kwa baadaye kwenye suala zima la elimu.Elimu haitakiwi kuchanganywa na mambo mengine kwani mwisho wake ni kushindwa vibaya, hivyo wanaotaka kusoma waangalie mbele kwanza na kuachana na mambo ya simu kwani hizo watazitumia tu wakishamaliza masomo. Ni mimi Upendo mkereketwa wa Elimu.

Mwanafunzi anayemiliki simu anasema, mimi sioni tatizo kwani ni kweli simu inanisaidia, katika masomo kwani siku hizi mambo yamebadilika mwalimu anaweza akafundisha jambo fulani, baadaye ukaperuzi kwenye mitandao ukapata kuelewa zaidi, Hao wanaosema wanafunzi tusimiliki simu za mkononi wanakosea, kwani wangeshauri matumizi mazuri ya simu za mkononi na sio kusema hazitusaidii, Wapo wanafunzi wanaotumia simu za mkononi vibaya lakini kwa yule anayejitambua hawezi kufanya hivyo. Mimi nawashauri wanafunzi tutumie simu katika maadili mazuri na si vinginevyo. Mwanafunzi Christina.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom