Uzoefu unaonyesha kuwa inapotokea misiba, baadhi ya watu huwa wanafanya kazi zao katika kuonyesha ufahari, badala ya kusaidia jamii, kinachojitokeza zaidi kwa baadhi ya watu, katika misiba ni kushindana kuvaa nguo za bei mbaya na nyingine zinazopingana na maadili ya Tanzania. Na kwa wakati huo unakuta watu hao hawakumbuki wakati marehemu alipokuwa anaumwa alihitaji msaada wa hali na mali ili apone lakini ijapokuwa walikuwa na uwezo wakumsaidia pesa za matibabu lakini hawakufanya hivyo.
Na sasa utakuta baadhi ya wanawake wamevaa nguo zinazowaacha sehemu kubwa ya mwili wazi kana kwamba wanakwenda disko, huku baadhi ya wanaume wakivaa hereni na suruali milegezo.Wapo Baadhi ya watu ambao walitengwa na ndugu jamaa na marafiki zao wakati wakiwa wagonjwa lakini siku ya misiba unakuta watu hao hao wanajimwaga msibani kwa wingi huku wakijitutumua kuonyesha uwezo wao katika kufanya mambo mbalimbali yanayohitajika pale msibani.
Baadhi ya watu wanasahau msibani siyo sehemu ya kuonyesha ufahari,umaarufu , wala uwezo wa mtu kifedha.NI VYEMA KUJITAMBUA ILI KUHESHIMU MAZINGIRA YA MSIBANI kwani wengine wanafanya ndiyo sehemu ya malumbano na majungu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni