Pages

Jumatano, Aprili 16, 2014

Asilimia 90 ya wanawake wanaosumbuliwa na saratani ya kizazi nchini wanafia majumbani.

Takwimu za saratani ya mlango wa kizazi kwa Tanzania inatisha kutokana na kuonyesha kuwa mwaka 2013 pekee, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ilipokea wanawake 1,216 sawa na asilimia 10 wanaosumbuliwa na ugonjwa huo. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo. (WAMA)  amesema asilimia 90 ya wanawake wanaosumbuliwa na saratani ya kizazi nchini wanafia majumbani, kwenye zahanati na vituo vya afya kutokana na dalili za ugonjwa huo kushindwa kugundulika mapema. 

Alitoa takwimu hiyo wakati wa uzinduzi wa uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi wilaya ya Bahi mkoani Dodoma. Amesema idadi hiyo ni kubwa hususani kwa wakati huu ambao teknolojia inawezesha kuchunguza, kugundua mapema na kutibu viashiria vyote  vya saratani hiyo, hivyo ni vyema wanawake kufika mapema kwenye vituo vya afya na kupimwa. Changamoto zilizopo ni tatizo la uelewa mdogo, imani potofu juu ya dalili za saratani na matibabu yake na unyanyapaa kutoka kwenye jamii.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom