Jumanne, Aprili 15, 2014

BAADHI YA WANAUME HAWAZINGATII SHERIA YA NDOA

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa 
Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), 
Valeria Msoka 
Katika maeneo mbalimbali ya nchi, utafiti wa  Chama cha Wanahabari Wanawake  Tanzania (TAMWA) umebaini tatizo kubwa la wanaume kutelekeza familia zao. Karibu wilaya zote ulikofanyika utafiti huu, umebaini kuwa tukio hili maranyingi linatokea msimu wa mavuno.Baadhi ya wanaume ukifika msimu huo huwa wanauza mazao yote yaliyopatikana katika familia na kwenda kunywa pombe au kuoa mwanamke mwingine .Hali hii inazifanya familia kukosa matunzo na hatimaye watoto kuacha shule na kukosa huduma stahiki za afya. 
Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 pamoja na mambo mengine inaeleza "Mke ana haki ya kupata matunzo kama chakula, mavazi, malazi na matibabu kutoka kwa mume ambayo hutegemea zaidi hali halisi ya uwezo wake, Inabainisha na kuelekeza wazi wajibu wa mume na mke katika ndoa" Lakini bado baadhi ya wanawake na watoto wanaendelea kunyanyasika kwa kukosa mahitaji muhimu kutokana na kutelekezwa na wanaume.Utafiti pia unaonyesha kuwa tatizo limeegemea katika msingi wa mfumo dume, unaweka umiliki wa mali za familia mikononi mwa baba, badala ya kuwa mikononi mwa mama au umiliki wa pamoja. Kina Mama ambao  waume zao  ndio wenye kauli ya mwisho juu ya mazao yapi yauzwe na fedha zitatumikaje. Wanaume wenye tabia hii waache mara moja.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom