Pages

Jumapili, Aprili 27, 2014

"Mume wangu anamtumia mtoto kunichunguza tabia"

Mimi ni mwanamke naitwa Alisa Nimeolewa hivi karibuni na mwanaume ambaye ana mtoto wa umri wa miaka 10, nampenda sana mume wangu na kuhusu suala la kuwa na mtoto alinieleza mapema hivyo nilikuwa najua na sikuwa na tatizo juu ya hilo na siku zote niliahidi kumpenda mtoto wa mume wangu kama wakwangu wa kumzaa. Tatizo limeanza hivi karibuni mume wangu huwa anamuambia huyu mtoto wake anichunguze kila ninachokifanya ikiwa ni pamoja na wageni wanaokuja pale nyumbani.

Kila anaporudi kutoka kazini huwa anamuita huyu mtoto na kumuuliza nani amekuja hapo nyumbani siku ya leo, na je kama mimi nilitoka pale nyumbani yaani mambo yote yanayofanyika pale nyumbani akirudi mume wangu anamuuliza mtoto, ukweli ni kwamba mimi hii tabia siipendi kwani nampenda sana mume wangu na sijawahi kumsaliti sasa ananishangaza katika hili nimeshajarubu kumueleza akaniambia, anafanya hivyo kwasababu ananipenda, yaani kwangu imekuwa ni kero naombeni ushauri wadau.

Maoni 1 :

emu-three alisema ...

Cha muhimu ni kutimiza wajibu wako tu , kwasababu huna hatia, na hutarajii kufanya ubaya au sio, ...basi mwisho wa siku atachoka,na kukupa shavu la kukuamini. MApenzi ya mwanzoni ndivyo yalivyo,...

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom