Pages

Jumatano, Aprili 23, 2014

Musoma na Bukoba Kuingia Dijitali Rasmi 01/05/2014

Miji ya Musoma na Bukoba kuwa katika mfumo wa Dijitali rasmi kuanzia Mei Mosi 2014. Mitambo ya Analojia kuzimwa usiku saa sita tarehe 30 Aprili 2014. Tanzania tayari imezima mitambo ya analojia katika miji 9 na hii sasa itafanya miji 11 nchini kuwa katika mfumo wa dijitali pekee. Dar es salaam, Arusha, Moshi, Mwanza, Tanga, Dodoma, Mbeya, Singida na Tabora tayari iko katika mfumo huo mpya wa Utangazaji.
Dunia nzima inatakiwa iwe imehama kutoka Analojia siku ya ukomo tarehe 17/06/2015.
Awamu ya pili Na ya mwisho ya uzimaji wa mitambo ya analojia ilianza mwezi machi 2014 ambapo utakamilika mwezi Novemba 2014. Baada ya hapo miji mingine iliyokuwa haina kabisa mfumo wa analojia itapata matangazo ya Tv kwa mara ya kwanza na katika mfumo wa dijitali kati ya Novemba hadi hiyo Juni na kuendelea.
Analojia ilikuwa inapatikana asilimia 24 tu ya Tanzania. Dijitali imefika karibu asilimia zaidi ya 30 baada ya miji ya Morogoro, Kigoma, Iringa na miji mingine kufungwa mitambo ya dijitali.
Maeneo mengi zaidi nchini watapata matangazo ya TV kuliko ilivyokuwa mwanzo.

Mifumo mingine ya Utangazaji inaendelea kama kawaida. Satelite (DSTV, ZUKU, AZAM na Free to air - madishi yote yasiyolipiwa), Cable Tv pia itaendelea pamoja na wale wanaotumia IPTV - Internet Protocol Tv - TV kupitia Internet. Mifumo hii iko dijitali tayari. Mfumo uliobadilika ni a"Terrestrial TV Broadcasting" pekee kupitia mitambo iliyosimikwa juu ya ardhi.

Tanzania inategemea kutimiza matakwa na maagizo ya ITU Shirika la Kimataifa la Umoja wa Mataifa linalosimamia Mawasiliano Duniani lililoelekeza kuwa ukomo wa mfumo wa analojia ni 17/06/2015.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom