Pages

Jumatano, Aprili 23, 2014

"SIKUTEGEMEA TANISA"


Haya yalikuwa ni zaidi ya mahaba niue, kwani Gody alitokea kumpenda sana Tanisa, siku zote alikuwa na ndoto ya kuja kuishi naye, kama unavyojua katika mapenzi unaweza ukawa umependa sana kwa moyo wako wote huku ukifikiri kuwa unayempenda naye anakupenda  lakini kumbe mwenzako akawa na mawazo tofauti. 

Gody alimuamini sana Tanisa na alikuwa tayari kwa lolote juu yake, ndipo siku moja ikiwa ni siku chache tokea Gody aende kujitambulisha kwa kina Tanisa na sasa walikuwa katika mikakati ya kufunga pingu za maisha. Siku hiyo Gody alikuwa katika matembezi yake na ndipo alipomuona Tanisa akiwa amesimama na kaka mmoja ambaye kwa kuwatizama tu alihisi kuna jambo tofauti basi alijisogeza haraka ili kutaka kufahamu ukweli wa kile alichokuwa anahisi.


Baada ya Tanisa kumuona Gody amefika pale alibadilika ghafla na kujifanya hamjui kitendo ambacho kilimchanganya sana Gody na kubaki ameshangaa,"Kweli Tanisa leo hii unanifanyia mimi hivi, mapenzi yote niliyonayo juu yako, tena tukiwa na malengo ya kuishi pamoja unanikana kwasababu ya huyu mwanaume, sikutegemea kama ungenitenda kiasi hiki" Tanisa alinyanyuka na kusema "Samahani sana kaka sikujui hunijui, tena naomba unikome,au wewe ni mwendawazimu".

 Gody  alibaki ameduwaa huku asiamini kile alichokuwa anakiona Tanisa na mwanaume wake waliondoka huku wakiwa wameshikana mikono na kumuacha Gody akiwa anasikitika sana "Sikutegemea Tanisa, nilimpenda sana, nilimfanyia kila jambo alilokuwa anataka leo hii amenitenda hivi, sikutegemea Tanisa". Katika maisha ya mapenzi kuwa makini sana kwani siyo kila anayekupenda anakupenda kutoka moyoni kumbuka unaweza kupenda usipopendwa mwisho wake ukabaki unaumia. Na Adela D Kavishe.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom