Pages

Ijumaa, Mei 09, 2014

HABARI ZILIZOCHUKUA UZITO KATIKA MAGAZETI YA LEO


GAZETI MWANANCHI
Dar es Salaam. Daktari wa Hospitali ya Mwananyamala, Saleh Kijangwa amejitokeza na kueleza jinsi alivyougua homa ya dengue ambayo imeukumba Mkoa wa Dar es Salaam.
“Niliumwa sana, nikadhani ni malaria na nikahisi imekuwa kali kiasi hicho kwa sababu sikuwahi kuugua malaria maishani mwangu. Nilipima magonjwa mengi lakini hakuna kilichoonekana,” alisemaDaktari huyo alisema kosa alilofanya ni kuamua kujitibu kwa kunywa dawa ya maumivu aina ya diclofenac ambayo kwa kawaida haipatani na maradhi hayo.
*****************************************************************************************************Dodoma. Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila jana aliibua tuhuma nzito bungeni akiwahusisha mawaziri wawili na Sh200 bilioni zilichotwa katika Akaunti ya Escrow, iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Tanesco na Kampuni ya kufua umeme ya IPTL.
Katika tuhuma hizo, alimuunganisha pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na vigogo wengine, wakiwamo wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wa Serikali, wote akiwataja tu kwa vyeo bila majina.
Mawaziri waliotajwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Fedha na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
********************************************************************************************
Singida. Dereva wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida, Juma Juma (52), amefariki dunia wakati akifanya mapenzi kwenye nyumba ya kulala wageni akiwa na mwanamke ambaye imedaiwa ni mhudumu wa baa.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela alisema tukio hilo lilitokea  Mei 3, saa 4:00 usiku chumba kwenye Na. S.2 cha nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Top Life New mjini Kiomboi.Alisema saa 6:00 usiku siku ya tukio hilo, dereva huyo alimuaga mpangaji wake kuwa anatoka mara moja na hangechelewa kurudi nyumbani kwa hiyo asifunge mlango wa mbele ya nyumba.
Alisema kuwa saa mbili baadaye, dereva huyo alionekana akiwa baa iliyoko kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni ambayo iko mita 50 kutoka nyumbani kwake.“Muda huo Juma alionekana akiwa na mmoja wa wahudumu wa baa hiyo aitwaye Agness Mayo (32) anayesadikiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi,” alisema.Kamwela alisema mhudumu huyo wa baa alitoweka Mei 4, mwaka huu baada ya kuaga kwamba anakwenda kanisani na kutorokea kusikojulika.
Hata hivyo, ufunguo wa chumba alicholala Juma zilikutwa chumba cha kulala wahudumu wenzake.Kamanda huyo alisema kuwa tangu siku Mei 3, chumba alicholala Juma hakikufunguliwa hadi Mei 5 mwaka huu wakati mwili wa dereva huyo ulipokutwa ukiwa umeharibika.“Uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta mhudumu aliyetoroka ili ahojiwe na kisha kufikishwa mahakamani endapo atabainika kuhusika na tukio,” alisema kamanda Kamwela.
***********************************************************************************************GAZETI TANZANIA DAIMA
JUMUIYA ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) imesema inaamini katiba mpya itapatikana bila kuwepo kwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).Hivyo, jumuiya hiyo imeitaka Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuacha kuwabembeleza na kuwaangukia UKAWA kurejea bungeni.
Kauli hiyo ilitolewa mjini Unguja jana na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka, katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisi kuu ya jumuiya hiyo.Alisema endapo theleuthi mbili ya pande mbili za Muungano itakosekana, hakutakuwa mkosi wala msiba badala yake katiba ya mwaka 1977 itaendelea kuliongoza taifa.
Kagasheki amvaa Pinda mgogoro wa Bukoba
MBUNGE wa Bukoba Mjini, Balozi Khamis Kagasheki (CCM), amemtuhumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kuwa ameshindwa kumchukulia hatua aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dk. Anatory Amani, ambaye amegoma kutii maagizo ya serikali.
Akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya ofisi ya waziri mkuu bungeni jana, Kagasheki alisema kuwa licha ya Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kushughulikia mgogoro huo, ofisi ya waziri mkuu imekuwa kimya.
Jackline Wolper arudia dini yake
MIEZI michache baada ya kuapa kwamba hatobadilisha tena dini kwa kwani kwa kufanya hivyo, ni sawa na kumchezea Mungu, mwigizaji mwenye nyota kali, Jackline Wolper, ameshindwa kusimamia kiapo hicho na kutangaza rasmi kurudia dini yake ya Kikristo.
Wolper ambaye alijikuta akislimu baada ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mfanyabiashara maarufu anayejulikana kwa jina la Dalaz na baadaye kumbwaga, amesema ameamua kurudi kwenye dini hiyo kutokana na kujiona kwamba aliwakosea sana wazazi wake ambao ni wacha Mungu.
“Kwa kweli nimekaa nikatafakari, nikaona ni bora nirudi kwenye dini yangu ukizingatia pia niliwakosea wazazi wangu ambao walinilea katika malezi ya kidini sana, lakini wakati nabadili hawakuwa na jinsi kwani waliheshimu maamuzi yangu japo kwa sasa nayajutia,” alisema mrembo huyo.
*********************************************************************************************

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom