Pages

Ijumaa, Mei 09, 2014

MAPENZI YA KWELI

Eric Thomas ambaye amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani ya mapafu, amelazimika kufunga ndoa na mpenzi wake Lindsay Thomas baada ya kuona hana dalili za kupona siku za karibuni. Kwa mujibu wa kituo cha Televisheni cha WXYZ, wawili hao walifungishwa ndoa na mchungaji kisha kufuatiwa na tafrija fupi iliyowahusisha wauguzi na madaktari hospitalini hapo. Maharusi wote walivalia mavazi rasmi ya harusi kama kofia ambazo zilifunika nywele zao.
Bibi Harusi hakuwa na tatizo lolote ila bwana harusi alikiri kuwa kofia hiyo ilificha athari za ugonjwa wake. "Nimelazimika kuvaa kofia kwaajili ya kufunika nywele zangu ambazo zinaonekana tayari zimeanza kunyonyoka, alisema Eric. Alieleza kuwa athari za ugonjwa huo kuwa si muhimu sana kama hatua aliyofikia ya kufunga ndoa na mtu anayempenda. Haya ni mapenzi ya kweli ni wachache sana ambao unakuta wanapendana wakati wa shida na raha.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom