Rais wa Liberia,Ellen Johson Sirleaf ametangaza amri ya kufungwa kwa shule zote nchini humo kama mpango wa taifa hilo wa kukabiliana na ugonjwa wa homa ya Ebola.
Mpango huo pia unashirikisha kuzitenga baadhi ya jamii zilizokatika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo.Hatua hiyo inajiri huku maafisa wa afya wakidaiwa kuzongwa na kazi katika mji mkuu wa Monrovia ambapo vyumba vya kuwatenga waathiriwa wa ugonjwa huo vimejaa.
Katika visa vingine wagonjwa wamelazimika kutibiwa nyumbani kutokana na ukosefu wa vituo vya kutoa matibabu.Ebola imeua sasa watu 672 magharibi mwa Afrika
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Thomas Fessy anasema huu ni mpango huo ambao mamlaka inaamini utapunguza mtagusano baina ya jamii na hivyo basi kusitisha kuenea zaidi kwa Ugonjwa huo unaoua.
Shule zote nchini humo zimefungwa ,na tayari wafanyikazi wa mashirika na Wizara za Serikali zisizo na umuhimu mkubwa wamepewa likizo ya siku 30.
Baadhi ya jamii zimetengwa-na kupewa madawa na chakula.
Serikali inajaribu kuzuia watu kutembea kutoka eneo moja hadi jingine ikiwa na imani kwamba watu walioathirika watajulikana na kutibiwa.
Vikosi vya usalama vimeagizwa kutekeleza hatua hiyo.Ebola huenea kwa kumgusa mtu aliyeambukizwa
Wakati huohuo baadhi ya raia wamepinga kubuniwa kwa eneo jipya la kuwatenga watu na kuwalazimu maafisa wa afya kuwatibu hadi wagonjwa 20 katika makaazi yao.
Bado haijulikani ni vipi serikali itafanikiwa kutekeleza hatua hiyo wakati ambapo kuna hofu na shauku.
Hadi kufikia sasa Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu 672 katika matifa matatu ya Afrika Magharibi yaani Liberia Sierra Leone na Guinea huku mtu mmoja akifariki nchini Nigeria.Liberia, Sierra Leone na Guinea zimeathirika pakubwa na Ebola.
Shirika la Marekani linalotoa misaada ya huduma kwa jamii (Peace Corps) limewaondoa mara moja wahudumu wao katika mataifa yaliyoathirika pakubwa Liberia, Sierra Leone na Guinea baada ya mmoja wao kupatikana ameambukizwa.
Kulingana na takwimu Ebola huua asilimia 90% ya watu walioambukizwa homa hiyo ambayo huchukua kuanzia siku 2-20 kujulikana iwapo mtu ameambukizwa.
Hiyo ndiyo sababu asilimia kubwa ya wahudumu wa afya waliokuwa wakiwatibu wagonjwa walidhania kuwa ilikuwa ni Malaria na hivyo kuambukizwa homa hiyo kali.Ugonjwa huu ulitubuka nchini Guinea mwezi Februari.Homa hiyo ilienea kwa haraka hadi Liberia na sasa Sierra Leone.CHANZO BBC SWAHILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni