Pages

Jumatano, Julai 16, 2014

"SIYO WATOTO PEKEE WANABAKWA HATA WANAWAKE WAKUBWA WANAFANYIWA VITENDO HIVYO"

Miongoni mwa mambo ambayo yanaendelea kuwaumiza vichwa wanaharakati mbalimbali wanaopambana na ukatili wa kijinsia  katika jamii yetu inayotuzunguka ni pamoja  na ubakaji, udhalilishaji wa kijinsia,ukeketaji, na utelekezaji wa familia. 

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) wamekuwa mstari wa mbele kupambana na vita hii ili kuhakikisha inapata ushindi.Hivyo muamko wa wanajamii kwasasa katika kuyaripoti matukio ya vitendo vya udhalilishaji, sasa unatia moyo angalau na kujenga matumaini kuwa inawezekana kutokomeza  kabisa aina zote za matendo ya ukatili wa kijinsia, ikiwemo ubakaji kwa wanawake na watoto. 


Kwa utafiti uliofanyika na Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA). Mwenyekiti wa Tume ya kurebisha  Sheria Jaji Mshibe Ali Bakar amesema  kuna mambo ambayo yamekuwa yakileta changamoto na kwamba sio watoto pekee ndiyo wanaobakwa  bali wapo na wanawake wakubwa wanaobakwa kwa vile hawapendi kwenda mahakamani kwa kuona aibu katika jamii inayowazunguka.

Amesema "Watoto ndiyo wanaofika mahakamani lakini wanawake wakubwa wanaogopa hivyo kubaki wakikaa kimya na kuvumilia vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa" Hata hivyo hali ya ubakaji bado ni kubwa na wanaoripoti ni kidogo ikilinganishwa na wanaobakwa. Hivyo ni vyema watu wakaamka na kuacha kuyafumbia macho mambo yote ya ukatili ikiwemo hili la ubakaji na elimu zaidi inahitajika kutolewa hasa kwa wanaume  kwa vile ndiyo wahusika wakuu wa vitendo vya udhalilishaji kijinsia.  

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

NIMEFURAHI NA TAMWA. ILA NAONA AJABU KWANINI HAWAATILII BLOGS ZINAZOWEKA PICHA ZA UCHI ZA WATANZANIA .JAMANI TUTETEE HAKI

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom