Pages

Alhamisi, Julai 17, 2014

Ujumbe wa leo kutoka kwa Isaack Shayo mwanafunzi bora kitaifa katika masomo ya Sayansi.

"Chanzo cha mimi kufaulu vizuri ni kujituma katika kusoma na pia kutafuta vitabu mbalimbali na pia kusumbua walimu ninapoona nimekwama, nimefurahi sana lakini pia mbali na kufanya hayo yote nimekuwa nikimshirikisha Mungu na kwa kusali sana naamini kumenisaidia kuweza kupata matokeo mazuri amesema Isaack (20) ambaye alihitimu Shule ya Sekondari ya St Joseph Cathedral.

 Isaack yupo kwenye kundi la watahiniwa 10 bora kitaifa kwa masomo ya Sayansi na pia kwenye kundi la wavulana bora kitaifa katika masomo hayo. Katika matokeo yaaliyotangazwa jana amepata alama 4. Fizikia amepata B+, Kemia A, Hisabati pamoja na Sayansi ya Kompyuta (somo la ziada) amepata A. HONGERA SANA KWA WALE WOTE WALIOFAULU VIZURI KIDATO CHA SITA. 

Maoni 1 :

Bila jina alisema ...

Congratulations! You deserve it. God bless you more.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom