Pages

Jumatano, Julai 23, 2014

UJUMBE KUTOKA KWA MHESHIMIWA LOWASSA "Elimu ya Tanzania ipo hoi taabani"Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, amesema elimu ya Tanzania ipo “hoi bin taaban” na ametaka iwekwe mikakati thabiti ya kuinusuru ili ijibu mahitaji ya ajira ya sasa.

“Leo hii Tanzania sisi ni akina nani tusiangalie elimu, lakini Mwalimu Nyerere, yeye alikwenda mbali zaidi na kuweka elimu ya kujitegemea ili iweze kujibu mahitaji ya Watanzania. Tunapaswa sana kutafakari kuhusu kufikiria suala la elimu. Sasa hivi elimu yetu ipo hoi bin taaban…imeundiwa tume na tume na kwa bahati mbaya taarifa zake hazijawekwa wazi, sasa sijui tatizo ni tume au serikali bado haijatekeleza ripoti hizo Elimu yetu ni lazima izingatie ajira, kwa bahati nchi yetu sasa hivi ina gesi ya kutosha. Na mahali pazuri pa kuelekeza gesi ni kwenye elimu, elimu bora itakayozingatia mahitaji ya sasa, la sivyo, gesi hii inaweza kuwa laana kwetu."Sehemu kubwa ambayo inaweza kuajiri vijana, wakiwamo wasomi wa aina aina mbalimbali wa makundi tofauti ni kwenye viwanda na kilimo.Tunatakiwa kujenga viwanda vingi na hasa vya pamba, hivi vinatoa ajira kwa waliomaliza darasa la saba, kidato cha nne, sita na hata vyuo vikuu,,”Tujenge viwanda hasa vya pamba (nguo) na fedha za gesi zipelekwe huko…sasa hivi tabaka la walio nacho na wasio nacho ni kubwa sana, tusipoliondoa hatutakuwa salama, tutakula nao sahani moja,”Alisema hayo wakati akiwa mgeni rasmi katika mkutano wa 25 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom