Wanaume wanatakiwa kuwa chanzo cha mabadiliko kwa kuwa mstari wa mbele kupima afya zao na kuacha tabia ya kuwaacha wanawake kwenda kupima peke yao hasa wakati wa ujauzito. Kwani kila mmoja atatambua afya yake na kama ameambukizwa ataanza matibabu mapema na hata kumkinga mtoto atayezaliwa . Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na programu ya TUNAJALI inaonyesha mwamko wa wanaume kuhudhuria kliniki na wake zao bado ni mdogo.
Ikizingatiwa kuwa wanawake kuongozana na wenzi wao kliniki ni muhimu sana kwani endapo kuna tatizo kwa pamoja watajua namna ya kupambana nalo. Kwani inawezekana Mama akapima akaonekana hajaathirika lakini Baba akapimwa akawa ameathirika au Mwanamke akawa ameathirika na Baba akawa hajaathirika hivyo ni muhimu kwenda pamoja katika vituo vya afya kupima na si kusubiri majibu ya vipimo vya mmoja wapo.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni