Ulikuwa ni usiku mtu mmoja akiwa anajiandaa kulala rafiki yake
akamwambia ni vyema kumshukuru Mungu kabla ya kulala, Mtu huyo akasema
"Najisikia kuchoka sana leo siwezi kusali, nitasali kesho wewe niombee
katika sala zako, basi akapanda kitandani na kulala wakati usingizi
ukiwa unampitia taratibu simu yake ya mkononi iliita alipokea na
aliyempigia alimtaka ajiandae anampitia waende club usiku huo, Mtu huyo
bila kupoteza muda alinyanyuka kitandani na kuanza kujiandaa haraka,
mwenzake aliyekuwa anasali alimtizama na kusema "Wewe si umesema
umechoka, mbona unajiandaa kwenda club".
Mtu huyo alikuwa anaitwa Mkelele, aliendelea kujiandaa, bila ya
kumsikiliza mwenzake, baada ya muda aliondoka kwenda club, huku
akimuacha rafiki yake akisikitika sana, alifika club na kujichanganya na
marafiki zake wengine ambapo walicheza na kunywa sana pombe, ilipofika
majira ya saa kumi za usiku walianza safari ya kurudi nyumbani, wakiwa
njiani walikutana na majambazi, hivyo walivamiwa na kunyang'anywa kila
kitu.
Wale majambazi walikuwa na silaha na kwa namna
walivyokuwa wamelewa walishindwa kupambana nao, hali ya Mkelele
ilikuwa mbaya sana kwani alipoteza fahamu alipozinduka alijikuta yupo
hospitalini, na aliyekuwa amesimama pembeni yake alikuwa ni yule rafiki
yake ambaye wanaishi pamoja alimtizama na kusema, "Najuta sana, kwani
yote haya yasingenikuta kama ningekusikiliza, nisamehe rafiki yangu
kwani shetani alinipitia".
Rafiki yake alitabasamu na kusema "Mungu ni kila kitu katika maisha
yetu,kwani hata kama umechoka kwa kiasi gani, angalau utaje neno moja tu
la kumshukuru kwani bila yeye hakuna linalowezekana, na pia
ulivyoondoka nilikuombea sana kwa Mungu akusamehe kwani ulikuwa hujui
utendalo , Mshukuru sana Mungu kwani amekupa nafasi nyingine" Basi tangu
siku hiyo Mkelele alimshirikisha Mungu katika kila jambo analofanya, na
maisha yake yanaendelea vizuri bila matatizo yoyote.nimatumaini yangu
kupitia simulizi hii fupi naimani kuna kitu ambacho utakuwa
umejifunza. NA ADELA DALLY KAVISHE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni