ILIPOISHIA
Sauti
ilizidi kupaa juu kwa ukali ikiambatana na kicheko cha cha ajabu, Renata
alipata hofu zaidi na wakati huu Charito alikuwa ameshikilia kisu kilichokuwa
kinatiririsha damu mithili ya maji yaliyofunguliwa bombani, alikuwa akimsogelea
Renata ambaye alipiga kelele kuomba msaada “Mamaaaa nakufaaa, nisaidieni jamani
nakufaaaaa Mungu wangu nisaidieeeeee mamaaaaaa” Ilikuwa ni sauti kali sana,
Kandida aliisikia sauti ya Renata akiwa chumbani na alishtuka moja kwa moja
alikimbilia chumbani kwa Renata.JE NINI KITAENDELEA USIKOSE SEHEMU YA 35.
INAPOENDELEA
Nilipofika
chumbani kwa Renata, nilimkuta akiwa amejikunyata huku akilia na kutetemeka
sana, nilipata hofu na mwili wangu ulisisimka kutokana na kuogopa nini kitakuwa
kimemsibu mdogo wangu, nilimsogelea na kumuuliza “Kuna nini Renata mbona
unapiga kelele kiasi hicho, umepatwa na nini wewe?”.
Renata alinishika na
kunikumbatia huku akisema “Dada, nimeota ndoto mbaya sana, shemeji na mchungaji
Mkombozi walikuwa wanataka kuniua, Dada naogopa mimi siwezi kulala peke yangu,
wameniambia bado mimi, yaani bado mimi watakula nyama yangu” Nilimsikiliza kwa
makini bila ya kuzungumza chochote huku moyoni mwangu nikiwaza “Mungu wangu,
nyumba hii inamatatizo gani, Renata atakuwa namashetani, kwani amekuwa akiongea
sana mambo ya ajabu, mbona mimi sijawahi kuona ubaya wa mume wangu wala
mchungaji Mkombozi, eeh Mungu nisaidie kwani kila siku ni afadhali ya jana”.
Nilikuwa nawaza huku nikimtizama Renata
aliyekuwa akiendelea kulia huku akisema “Dada, mimi nakuambia umezungukwa na
watu wabaya, mpigie simu mchungaji James aje kunichukua, mimi siwezi kulala
huku ndani.” Wakati huo ilikuwa ni majira ya saa tisa usiku, nilimtizama na
kusema “Renata hiyo ni ndoto mdogo wangu usiogope, na inatokana na wewe umekuwa
ukiwaza mambo mabaya kuhusu shemeji yako, sasa muda huu unataka nimuite mchungaji ni kitu ambacho
hakiwezekani, wewe lala halafu kesho ukitoka tu shule, tunaenda kwa mchungaji
James” Nilimbembeleza lakini alikataa kabisa kulala mwenyewe sikuhiyo ilinibidi
nilale naye hadi ilipofika asubuhi ambapo mume wangu Charito alikuja chumbani
na kutuamsha kwani tayari ulikuwa ni muda wa Renata na Tumaini kujiandaa kwenda shule.
Haraka niliamka kwenda kuandaa kifungua kinywa
na wakati huo Renata na Tumaini walikuwa
wakijiandaa, Charito aliwahi kuondoka
sikuhiyo, huku akisema “Leo kuna kazi natakiwa niwahi kuifanya, hivyo hata chai
sintoweza kunywa, kwani naweza kuchelewa” Aliongea huku akiwa anaondoka,
nilimaliza kuandaa kifungua kinywa, na baadaye tulijumuika na kunywa chai
pamoja, sikuhiyo Renata alikuwa mkimya sana kwani hakutaka kuzungumza chochote
kama ilivyokawaida nilimtizama na kusema “Renata vipi, mdogo wangu unajisikiaje
hali yako” Alinitizama nakusema “Mimi mzima dada hakuna tatizo”.
Aliitikia kwa
sauti ya unyonge na ghafla alisimama huku akiwa bado hajamaliza kunywa chain a kulekea
mlango wa kutoka nje nilishindwa kumuelewa na kuuliza “Mbona haujamaliza kunywa
chai wewe unaenda wapi, subiri nitawapeleka shule pamoja na mdogo wako
unanisikia wewe.” Renata aliendelea kuondoka bila ya kugeuka nyuma na
hakunijibu chochote. Nilimuacha nakuhisi labda kuna kitu amechukia, na hivyo
ameamua kwenda kukaa nje na kutusubiri hivyo niliendelea kunywa chai na Tumaini
huku nikiwaza “Huyu Renata sijui anamatatizo gani, jamani mbona Napata wasiwasi
sana juu ya huyu mtoto” Baada ya Muda kama dakika tano kupita tokea Renata
atake nje, nikiwa najiandaa kunyanyuka na kuondoa vyombo nilisikia kelele za
watu nje kwa mbali lakini sikuzitilia maanani.
Baadaye niliona kelele zinazidi ilinibidi
nitoke nje na kutaka kujua nini kinaendelea nilipotoka kwanza nilitizama huku
na kule pale barazazni ambapo nilijua Renata angekuwepo lakini sikumuona
nilipotizama kwenye geti lilikuwa halijafungwa lipo wazi moja kwa moja nilitoka nje na kuona umati
mkubwa watu wakiwa wamezunguka huku na kule wengine wakisema "ajali, jamani,
halafu aliyegonga amekimbia hata namba ya gari hakuna aliyekariri" nilimuona
Mama mmoja ambaye nilikuwa nikifahamiana naye pale mtaani alinisogelea huku
akisema Kandida, jamani Kandida uwiiiiii jamani….. nilishtuka sana kumuona
katika hali ile haraka nilisogea kwenye ule umati na kutizama aliyekuwa
amegongwa na gari masikini alikuwa ni
Renata mdogo wangu, nilipiga kelele huku nikiwa nimeweka mikono yangu kichwani
sikuamini nilichokuwa nakiona damu zilikuwa zimetapakaa pale chini, nilisogea
karibu zaidi na kujikuta miguu yangu yote imeishiwa nguvu huku nikitetemeka
sana baadhi ya kina mama walinishika lakini hakikusaidia hatimaye nilianguka
chini na kupoteza fahamu.
Baadaye nilizinduka na kujikuta nikiwa nyumbani
ambapo pembeni yangu alikuwepo Charito mume wangu nilijikuta naanza kulia kwa
uchungu sana “Masikini mdogo wangu, Renata wangu jamani, inaniuma sana mdogo wangu, tulikuwa
tunakunywa chai pamoja asubuhi, yalaiti ningekushika mkono usitoke nje, mdogo
wangu moyo wangu unaumia sana jamani”
Nililia sana kwani nilikuwa siamini kama Renata amefariki, Charito
alijitahidi kunibembeleza na kusema “ Nyamaza mke wangu usilie mke wangu, yote
hiyo ni mipango ya Mungu, sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi” USIKOSE
SEHEMU YA 36 sasa tutaanza kuipeleka haraka hadi mwisho wake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni