Jumatano, Oktoba 22, 2014

SIMULIZI YA MAISHA "USILIE NADIA SEHEMU YA 17 NA 18"

 ILIPOISHIA
Hilo likawa neno lake la mwisho kwa kiingereza akaanza kuzungumza kiarabu cha ndani kabisa. Alinivuta lakini sikutaka kumfuata. Niliendelea kung’ang’ania vyuma nilivyokuwa nimeshikilia. Lakini nilijua tu ni mfa maji haishi kutapatapa…….” Akasita kisha akaendelea, “Yaani nimesema maji nd’o nakumbuka tumenunua maji na hadi sasa hatujanywa!! Duh yasije yakawa ya moto tena.” Alisema Nadia kisha akachukua maji nami nikatwaa yangu, hakika makoo yalikuwa yamekaua haswaa!!USIKOSE SEHEMU YA 17

SEHEMU YA KUMI NA SABA

“Katika maisha wanadamu huwa ni wagumu sana kuamini kuwa Mungu yupo hasahasa wakati wa shida ama tatizo kubwa. Mungu hukumbukwa wakati wa raha tu. Utawasikia maharusi wakimshukuru Mungu kwa kuwafanikishia jambo hilo walilolingoja kwa muda mrefu lakini ni nadra sana kuwasikia wafiwa wakimshukuru Mungu waziwazi kwa kumtwaa mojawapo kati ya wapendwa wao!! Wanadamu sisi watu wa ajabu sana!! Nawakumbuka rafiki zangu wengi tu walivyofeli masomo yao hawakumwambia Mungu asante kama walivyofanya baada ya kufaulu!!” Nadia alinieleza maneno yale baada ya kuwa amekunywa nusu chupa ya yale maji. Nami nikatikisa kichwa kumuunga mkono.

“Hata mimi ni mmojawao, mmoja kati ya wasiomkumbuka na kumuamini Mungu wawapo katika shida ngumu. Badala yake kutarajia miujiza ya kidunia. Maana katika giza lile ambalo nilikuwa kisha yule muuaji akanikamata miguu sikutarajia lolote linaweza kufanyika kwa muujiza wa Mungu na badala yake niliendelea kuamini kuwa ni mimi pekee wa kuweza kuiokoa nafsi yangu. 

Niliendelea kutapatapa huku na kule nikiling’ang’ania chuma ambalo lilibaki kuwa muhimili wangu mkuu, na yeye aliendelea kunivuta huku akizidi kuweka viapo vikali vya kuniua kwa kunikatakata. Labda ulikuwa wakati wa kujikabidhi kwa Mungu lakini ningeanza vipi kuamini kuwa Mungu alikuwa upande wangu wakati kila baya linalotokea aliwashindia maadui zangu na akiniacha mimi katika majeraha? Nikajiaminisha kuwa yule hakuwa Mungu wangu bali Mungu wa maadui zangu.

Naam!! Huenda aliisikia sauti yangu, labda alingoja niwe katika wakati mgumu kama ule nd’o aweze kujionyesha kwangu!! Lile chuma ambalo nilikuwa nalitegemea sasa lilianza kulegea kutokana na kuvutwa sana na yule mzee wa kiarabu tuliyezoea kumuita masta. Hapo sasa nikakata tamaa, nikataka kujiachia lakini nafsi ikagoma kukata tamaa nikaendelea kushikilia japo nilikuwa nazidi kulisikia likisogea na mimi.

Mara likafyatuka!!

Nilichoweza kukisikia ni yowe la hofu kutoka kwa yule mwarabu, na baada ya hapo maji yalitusomba kwa nguvu mno na kisha kuanza kusdafiri nasi, ni hapo ndipo nikatambua kuwa chuma niliyokuwa nimeshikilia ilikuwa ni ufunguo wa aidha tanki la maji ama chochote kile. Lakini ajabu ni uwingi wa maji yale, nikajishukuru kwa kutokuwa mvivu kujifunza kuogelea enzi hizo nikitumikia uvuvi nyumbani kwao Desmund, nilikata maji kwa mwendo mkali, hofu ikiwa imetanda hasahasa lile giza nene, giza likiwa limetawala. Nilijigonga huku na kule lakini sikubadili azma yangu ya kutapatapa kama nitakufa nife nikiwa najaribu!! Baada ya kuogelea kwa dakika kadhaa hatimaye niliweza kuona mwanga. Hapakuwa na giza tena, niliangaza kushoto na kulia baada ya kunyanyua kichwa changu, nikawaona watu kwa mbali, hivyo nikatambua kuwa sikuwa mbali sana kutoka katika ufukwe. Hofu nyingine ilikuwa juu ya nchi ambayo ningeweza kuwepo na watu wa pale ufukweni, isijekuwa ni walewakle waliokuwa wametuteka wakanikamata tena. Nikazama tena majini na kuanza kupiga mbizi. Na nilipoibuka tena ndipo nilipokutana na maajabu makubwa ambayo sikuyatarajia hata kidogo!!

Nikaona PANTONI…..lilelile la Kigamboni!!

Kwa hiyo pale tulikuwa Dar esa salaam!!

Nilistaajabu huku nikiendelea kukata maji, sikujua hata ni wapi nilitokea hadi kufika pale nilipokuwa, lakini nilitilia mashaka maggorofa kadhaa yaliyokuwa kandokando na bahari ya hindi.  Nikaufikia ufukwe, mavazi yangu yakiwa tepetepe, ubize wa watu jijini Dar es salaam ukanisaidia sana, hakuna aliyekuwa na habari na mwenzake katika ufukwe ule. Nilijituliza huku nikitafakari ni kipi kinafuata katika maisha yangu baada ya Mungu kuniepusha na mauti yale?

Hakika ni Mungu tu, maana kwa uweza wangu hakuna ambalo ningeweza kufanya.

Jua likapiga na upepo ukapuliza mavazi yangu yakapata hali ya ukavu kiasi!!

Na akili nayo ikachangamka na kutambua kuwa kuna uwezekano mkubwa sana wale watu watakuwa wakinitafuta. Na iwapo wakinikamata wataniua maana kuna siri tayari nilikuwa nimezijua, utumwa katika nchi huru, tena utumwa wenye adhabu nzito ndani yake. Uuzaji wa madawa ya kulevya!!

Nikasimama wima, walau nilikuwa katika jiji ambalo nilikuwa nalifahamu, lakini ni jiji ambalo bila kuwa na pesa hauna maana ya kuwa hapo nadhani unalijua vyema, nami sikuwa na nauli wala mtu ninayemfahamu pale. Nikiwa wima nikajiuliza niende wapi, mwisho nikaamua kuelekea Vijibweni, ni huku tuliwahi kuishi na familia yangu kabla sijaamua kuasi na kuungana na Desmund katika mahusiano ya mashaka, mateso na karaha tupu huku yakiichafua historia yangu jumla. Nilipiga hatua moja baada ya nyingine, kutoka kivukoni hadi Kibada si karibu hata kidogo nililazimika kutembea sana. Hatimaye nikaifikia ile nyumba ambayo zamani nilikuwa nikikohoa kidogo tu nasikilizwa, nyumba ambayo mlinzi alikuwa akiniogopa na kuniheshimu zaidi ya mbwa mkali. Nyumba ambayo familia yenye upendo na amani iliishi humo. Nikainama chini na kujitazama, sikuwa na viatu na nguo niliyovaa ilikuwa imechakaa, nikajifikiria jinsi kichwa changu kisichokuwa na nywele nyingi jinsi kisivyotamanisha hata kukitazama. Kwa unyonge kabisa nikapiga hatua tena nikalifikia geti.

Nikajipa moyo kuwa labda habari za kwenda Saudi Arabia ni uongo mtupu familia yangu itakuwepo.

Labda hata habari za mama kufariki ni uongo vilevile alikuwa hai na wote walikuwa ndani, labda hata mlinzi aitwaye Hamduni nitamkuta na ataniheshimu tena.

Wakati naduwaa mara geti lilifunguliwa ghafla, akatoka mlinzi akiwa na bunduki aina ya gobole mkononi. Alikuwa ameikunja sura yake akinitazama mimi.

“Wewe ni nani ana unataka nini hapa?” alinikoromea! Nilikuwa katika mshtuko bado nikabaki kumwangalia badala ya kumjibu, akanirukia na kunikwida na kisha kurudia swali lilelile

“Naitwa Mariam!” nilimjibu.

“Sijakuuliza jina kichaa wewe, unafanya nini hapa muda huu?” aliniuliza kwa jazba. Kabla sijajibu akaendelea, “Hapa haturuhusu hayo mambo yenu ya kuombaomba sijui” alisema lakini mara akanikazia macho katika kifua changu!! Nami nikajitazama, nilikuwa natokwa damu.

“Umekuwaje binti!!” sasa aliniuliza kwa upole.

“Naitwa Mariam, wazazi wangu wanaishi katika nyumba hii”

“Wazazi wako?...maskini madawa ya kulevya kila siku wanakataza maskini. Binti mzuri kama huyu na yeye yamemwathiri looh!! Kijana taifa la kesho huu usemi ufutwe sasa.” Alilalamika peke yake, nikajua anahisi mimi nimeathirika na madawa.

“Mzee Barghash ni baba yangu.” Niliongezea.

“Binti….njia ile pale waweza kwenda zako mbali na hapa.”

“Babu sijachanganyikiwa, situmii madawa ya kulevya, nina akili zangu timamu, niulize lolote nami nitakujibu!! Tafadhali nisaidie nionane nao.”

“Binti leo tarehe ngapi mwezi wa ngapi? Na ni mwaka gani huu achana na tarehe kwanza.” Aliniuliza kama kunipima akili. Hakika alikuwa amenipata vilivyo, sikujua hata huo ulikuwa mwaka gani na sikujua hata nimekaa kule mafichoni kwa muda gani. Lakini nikajitahidi niweze kujibu ili aweze kuniamini.

Nikajiaminisha kuwa huenda hata mwaka mmoja haujaisha tangu nitupwe kule. Nikaamua kukadiria kuwa ulipita mwaka

“Mwaka 2010…”

“Yesu wangu weee!! Binti toka na upotee mbele yangu mara moja nasema.”

“Babu nipe nafasi ya mwisho. Nisikilize tafadhali.”

Wakati anataka kunitishia bunduki mara mtu mmoja akatokea getini, na kumshangaa yule mzee.

“Kababu huyu ni nani? Bona chafu chafu tu navaa uchi hapa” sauti ya mama wa kihindi. Ikakoroma huku akinitazama kwa sekunde moja huku sekunde nyingine akimtazama mlinzi. Ile hali ya kuhangaika kuzungumza Kiswahili ikanipa upenyo wa kujaribu bahati yangu ya kuuthibitishia umma kuwa sikuwa kichaa.

“Excuse me madame! Can I talk to you..pleasee!!” nilimsihi kwa lugha ya kiingereza, hapo akashtuka na kisha kuniuliza kwa kiingereza huku akiwa na wasiwasi na mlinzi naye akinishangaa.

“Wewe ni nani.’ Akaniuliza, nikajieleza vyema ubin wangu.

“Ooooh!! Baba yako alituuzia nyumba hii miaka mingi sasa hadi leo 2010 ni muda sana. Kumbe wewe ni mtoto wake, nini kimekutokea?” alinieleza na ni hapo nikatambua kuwa nimekaa kule sirini kwa miaka miwili tangu 2009 na huo mwaka ulikuwa 2011. Nikabaki kinywa wazi. Hapakuwa na jipya nikajaribu kuulizia kuhusu majirani, mama yule hakuwa akimfahamu hata mmoja.

Kisha akaamuru geti likafungwa!!

Nikatakiwa kupotea eneo lile.

Nikatii lakini nikamwomba mlinzi kidogo anisikilize.

“Jizungushe pita baada ya dakika kumi apotee.” Aliniambia, nikajiondokea. Nikapita huku na kule kama nitakuta wale majirani wa miaka hiyo lakini haikuwa hivyo, palikuwa na watu wagenmi tu!!

Baada ya dakika kumi nikarejea. Nikamwomba mlinzi aniazime simu yake nipige. Aliniangalia kwa mashaka nami nikagundua hofu yake.

“Nikutajie namba unipigie hizo namba tafadhali nakuomba.” Nilimsihi, akanielewa.

Nikajaribu kuvuta kumbukumbu, nikataja na kungoja majibu.

Simu ikaanza kuita!! Mara ya kwanza haikupokelewa!!

Mara ya pili ikapokelewa na mwanaume, jambo ambalo sikulitarajia.

Mlinzi akaniamini akanipa simu nizungumze huku akiiweka sawa bunduki yake, bila shaka kitisho nisikimbie na simu yake.

“Samahani, naomba kuongea na nani huyu? Naomba kuongea na mwenye simu kakangu.” Nilijikuta nasema.

“Mimi ndiye mwenye simu aisee.” Alinijibu kwa jeuri.

Nikaishiwa usemi lakini mara nikamsikia akisema maneno chinichini na hatimaye akaanza kuongea msichana.

“Halo! Samahani nikumbushe jina lako tafadhali.”

“Yaani wewe unapiga na hujui unayempigia.”

“Samahani wewe ni Jesca.”

“Kwani wewe unampigia nani?” aliniuliza na mlinzi naye alikunja sura akionyesha kujutia pesa ilivyokuwa inateketea katika simu yake.

“Nampigia Jesca tafadhali.” Nilisihi.

“Ni mimi nini shida na nani mwenzangu?”

“Jesca mimi Mariam, mimi Nadia Jesca!!! Jesca kama ni wewe kweli tambua kuwa nipo katika shida kubwa.”

“Nadiaaaa!!! Nadiaaaa!!!” alihamanika huko alipokuwa.

Simu nayo ikakatika!!

Mlinzi akaanza kulaumu, mara simu ikaita kwa namba mpya tofauti na ya Jesca, mlinzi akapokea.

Alikuwa Jesca.

“Nadia nilijua haujafa, nilijua wamekusingizia Nadia, nilijua ni njama….nililia Nadia, nililia sana lakini sikuwa tayari kusema ulazwe pema peponi, sikuwa tayari Nadia. Sauti yako ipo hai Nadia, nakupenda Nadia wangu, upo wapi Nadia.” Aliongea kwa hisia kali Jesca, machozi yakaanza kunibubujika.

“Nipo kama sipo, nipo kama mzimu, sina nguo za kuvaa, sina chakula, sina mahali pa kuishi. Ni afadhali ningekuwa katika kambi za wakimbizi. Jesca labda ni bora ningekuwa nimekufa, lakini ninayopitia ni zaidi ya mahangaiko. Jesca nakupenda sana na namba yako haikufutika katika kichwa changu kamwe. Nilikwambia ni wewe pekee ndugu yangu katika dunia hii. “

“Mtanimalizia chaji yangu!!” alilalamika mlinzi.

‘Jesca upo wapi kwani.”

“Nipo mlimani mpenzi. Nipo huku chuoni.”

“Jesca jamani!!! Hadi umefika chuo, mimi nipo huku Kibada, kama nilivyokwambia sina hali.”

“Kibada ni wapi??”

“Kigamboni…” nilimjibu nikamsikia akimuuliza yule mvulana aliyepokera simu mara ya kwanza.

“Baby Kibada unapajua”..kisha baada ya dakika kadhaa akaniambia, “tunakuja huko muda si mrefu eti utungojee Kigamboni huohuo upande wa pili..”

“Jesca natamani ungepewa macho, unione nilivyovimba miguu, upewe na tumbo langu uisikie hii njaa kali inayioishi humu, Jesca sitaweza kufika Kigamboni. Nitafia njiani!!” nilimnweleza. Nikamsikia akilia kwa kwikwi kutoka upande wa pili.

“Basi tunakuja hadi huko!! Usijali.” Aliniambia.

“Sawa mtatumia namba hii babu ataniambia.” Nilihitimisha.

Kisha nikazungumza na babu akakubaliana na mimi, nikaahidi kuwa wakifika nitampa chochote kitu atie mfukoni. Hapo nikamteka.

Nikaondoka pale na kujiweka mbali kidogo, nilipokaa chini nikakumbuka kumshukuru Mungu wangu!!! Alikuwa akinionyesha miujiza.

Baada ya masaa mawili na nusu hatimaye nikaona gari likisimama kwa mbali, babu akanipungia mkono. Nikakimbia mbio kwenda alipokuwa.

“Wapo ndani ya gari ile, usisahau chochote kitu!!”

Hapo hapo nikatimua mbio, mara mlango wa gari ukafunguliwa haraka akatoka binti akiwa amevaa kisasa sana, sketi fupi mno na viatu virefu. Akaweka urembo wake kando akavua viatu na kuanza kutimua mbio.

Harufu ya upendo ikasafiri na kuzifikia pua zangu, macho yanayomaanisha yanachotazama yakanieleza kuwa yule alikuwa Jesca. Naam! Hatimaye tukakutana ana kwa ana tukarukiana na kukumbatiana kwa nguvu, hiyo haikutosha Jesca akajisahau kuwa mimi nina njaa akanirukia tukaanguka chini lakini furaha haikupotea hata kidogo!!

Jesca alikuwa analia na machozi yake yaliangukia katika mabega yangu!!

Alikuwa amekuwa mdada mkubwa tena wa kisasa!!

Baada ya kusalimiana nikamkumbuka babu, Jesca akanipatia noti mbili nyekundu nikampelekea, mzee hakuamini lakini nadhani alitambua kuwa wema wake na imani yake kwangu vilikuwa vikubwa sana!!

“Bryan….anaitwa Mariam ni dada yangu. Na…Mariam huyu anaitwa Bryan ni mchumba wangu. Mengi tutayafahamu mbele kwa mbele.” Alitambulisha Jesca. Kisha nikapakizwa ndani ya gari tukaondoka!!

Wanasema kuwa baada ya dhiki ni faraja lakini kwa Nadia mimi kila baada ya dhiki ilikuwa inakuja dhiki nyingine inayofanana na faraja kisha inanisulubu. Hata hapa nilipokuwa sikutaka kujidanganya kuwa nimefika katika kikomo cha mateso!! Lakini walau nilikuwa katika mikono ya Jesca, na hapo niliweza tena ku….” Nadia akanitazama kisha akatabasamu!! Nikaelewa alikuwa anamaanisha nini kuikatisha ile kauli.

“Hee!! Yaani kumbe unanisikiliza tu hata kusema Nadia twende kula muda umefika aa mwanaume mbaya wewe dah!! Mwone!! Mi nina njaa mwenzako sio siri, ile kapuchino yote imamemalizika tumboni…”

“Niwapigie simu walete huku ama..”

“Hamna hawa wakileta huku huwa wanapunja sana. Twende hukohuko yaani wakinipunja tu naenda jikoni mwenyewe kujipakulia.” Alitania Nadia, tukajikuta tunacheka wote.

“Haya basi nipishe nibadili nguo mwenzako.’ Aliniomba, nami nikatoka nje ya chumba chake na kwenda katika chumba changu. 

Huko chumbani wakati na mimi nabadili nguo nilikuwa nahangaika na utata wa simulizi hiyo yenye maswali mengi!!

Sasa Jesca na Nadia wamekutana Dar!! Hivi huu ndo mwisho wa simulizi ama? Lakini haiwezi kuisha maana hali niliyomkuta nayo Nadia Musoma haikuwa ya kawaida hata kidogo sasa alirudi lini Musoma na ni kwanini nilimkuta katika hali ile??

INAPOENDELA  SEHEMU YA 18
“Katika maisha wanadamu huwa ni wagumu sana kuamini kuwa Mungu yupo hasahasa wakati wa shida ama tatizo kubwa. Mungu hukumbukwa wakati wa raha tu. Utawasikia maharusi wakimshukuru Mungu kwa kuwafanikishia jambo hilo walilolingoja kwa muda mrefu lakini ni nadra sana kuwasikia wafiwa wakimshukuru Mungu waziwazi kwa kumtwaa mojawapo kati ya wapendwa wao!! Wanadamu sisi watu wa ajabu sana!! 

Nawakumbuka rafiki zangu wengi tu walivyofeli masomo yao hawakumwambia Mungu asante kama walivyofanya baada ya kufaulu!!” Nadia alinieleza maneno yale baada ya kuwa amekunywa nusu chupa ya yale maji. Nami nikatikisa kichwa kumuunga mkono.

Sasa Jesca na Nadia wamekutana Dar!! Hivi huu ndo mwisho wa simulizi ama? Lakini haiwezi kuisha maana hali niliyomkuta nayo Nadia Musoma haikuwa ya kawaida hata kidogo sasa alirudi lini Musoma na ni kwanini nilimkuta katika hali ile?? USIKOSE SEHEMU YA 19

Maoni 2 :

Bila jina alisema ...

Duuh..maskin Nadia. Ahsante Adella kwa simuliz tamu.Mungu awe nawe

ADELA KAVISHE alisema ...

MDAU SEHEMU YA 17 NA 18 NIMEUNGANISHA PAMOJA SASA MWANZONI ILIWEKWA KIMAKOSA SAMAHANI KWA USUMBUFU TUENDELEE KUWA PAMOJA

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom