Jumatatu, Julai 21, 2014

"Wanaume wanatakiwa kuacha tabia ya kuwaacha wanawake wajawazito kwenda kupima VVU peke yao."


Wanaume wanatakiwa kuwa chanzo cha mabadiliko kwa kuwa mstari wa mbele kupima afya zao na kuacha tabia ya kuwaacha wanawake kwenda kupima peke yao hasa wakati wa ujauzito. Kwani kila mmoja atatambua afya yake na kama ameambukizwa ataanza matibabu mapema na hata kumkinga mtoto atayezaliwa . Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na programu ya TUNAJALI inaonyesha mwamko wa wanaume kuhudhuria kliniki na wake zao bado ni mdogo. 

Ikizingatiwa kuwa wanawake kuongozana na wenzi wao kliniki ni muhimu sana kwani endapo kuna tatizo kwa pamoja watajua namna ya kupambana nalo. Kwani inawezekana Mama akapima akaonekana hajaathirika lakini Baba akapimwa akawa ameathirika au Mwanamke akawa ameathirika na Baba akawa hajaathirika hivyo ni muhimu kwenda pamoja katika vituo vya afya kupima na si kusubiri majibu ya vipimo vya mmoja wapo.

SOMA SIMULIZI YA MAISHA: USILIE NADIA SEHEMU YA KWANZA UTAISOMA HAPA HADI MWISHO WAKE



SEHEMU YA KWANZA
Mwendo wa kutoka nyumba ya kulala wageni tuliyolal usiku uliopita haukuwa mkubwa sana hadi kuifikia staendi kuu ya mjini Musoma ambayo ujenzi wake ulikuwa unaendelea bado licha ya kwamba ilikuwa imeanza kutumika. Mara yangu ya mwisho kuingia katika mji huo ambao ni makao makuu ya mkoa wa Mara kituo cha mabasi bado kilikuwa kipo katikati ya mji. 

TULIPOFIKA kituo cha mabasi tuliangaza huku na kule huku tukikwepa usumbufu wa ‘wapiga debe’ wa kutuchagulia gari la kupanda huku wakitoa sifa kedekede kuhusu gari wanalolipigia debe.
“Tupande Zacharia Coach” alininong’oneza binti yule huku akinielekeza mahali zilipo ofisi zao. Tukajongea huku kila mmoja akiwa ametundika begi lake mgongoni. Nilimsaidia kubeba kifurushi kimojawapo.

Baada ya kupata tikiti zetu mbili ambazo zilituruhusu kuketi pamoja katika basi lenye hadhi ya V.IP, tulijongea upesi garini japo muda wa kuondoka ulikuwa haujafika. Lakini hatukuwa na jambo lolote la kutufanya tukae nje.

“Naomba nikae dirishani kaka” aliniomba, nikamruhusu nami nikaketi mkono wake wa kushoto, hapa sasa niliweza kumchunguza kidogo kwa macho ya kuibia ibia nywele zake jinsi zilivyokuwa zimenyonyoka, huenda ni kwa sababu ya kukosa matunzo. Uso wake ulikuwa umechujuka na ile rangi yake ya asili ilikuwa imetoweka. Alikuwa na mabaka mabaka yasiyokuwa rasmi na ambayo nilikuwa sijajua sababu yake.

KUELEKEA UCHAGUZI 2015 "Walimu wamtangaza Makamba urais 2015"



Walimu vijana wamezindua rasmi mtandao wao na kusema wanaunga mkono uamuzi wa Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, wa kutangaza nia ya kugombea urais mwakani, ambayo wanaamini itatimiza ndoto ya vijana ya kujiongoza na kujitawala nchini.

Mtandao huo ujulikanao kama 'Mtandao wa Walimu Vijana Tanzania', ulizinduliwa baada ya viongozi wake kuchaguliwa katika mkutano uliofanyika mjini Dodoma jana.

Mratibu wa Mtandao huo, Frederick Mwakisambwe, akisoma maazimio katika mkutano huo, alisema wana wajibu wa kuvaa viatu vya mwalimu mwenzao, Baba wa Taifa, hayati Julius Nyerere, siyo tu kushiriki kugombea uongozi, pia kuwaelewesha Watanzania aina ya kiongozi bora na makini atakayewafaa na kuwavusha salama kwenye changamoto za kizazi kipya.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom