Vitamini A itokanayo na bamia husaidia kuupa mwili wako kinga ya kupigana na
maradhi. Kwa wenye matatizo ya kuona, kula bamia mara kwa mara
kutaimairisha mwanga katika macho yako.
Wingi wa vitamini A huzuia maradhi yatokanayo na virusi kama mafua.
Uteute uliomo katika bamia husaidia kuunda tishu za mwili na ngozi. Watu
wenye ngozi laini na zinazoteleza wana kiwango kikubwa cha ute ambacho husaidia
kujenga ngozi.
Ulaji wa mboga za majani kama bamia, husaidia katika kulinda mapafu na saratani za mdomo. Bamia zina wingi wa vitamini K ambayo husaidia kuimarisha mifupa na kuganda kwa damu.
Maoni 1 :
Ahsante,lakin naomba kujua jinsi ya kutayarisha hzo bamia??
Chapisha Maoni