Mkazi mmoja wa Miembe Saba wilayani Kibaha mkoani Pwani
amekamatwa na polisi akituhumiwa kuwabaka watoto wake wawili wadogo kwa
zaidi ya miaka miwili sasa.Habari zilizolifikia gazeti hili, zilisema kuwa
katika tukio hilo ambalo limethibitishwa na polisi na watoto wenyewe,
baba huyo alianza kuwafanyia binti zake vitendo hivyo mwaka 2013 kwa
siku ambazo mkewe ambaye nimama wa wasichana hao hakuwapo hadi usiku wa
Machi 19, mwaka huu. Kwa sasa tunayahifadhi majina ya familia hiyo.
Watoto hao mmoja mwenye umri wa miaka 15 anayesoma
darasa la saba na mdogo wake mwenye umri wa miaka 11 aliyeanza kubakwa
akiwa darasa la tatu.Kwa mujibu wa watoto hao, baba huyo alikuwa
anamuita mmoja wa watoto wake chumbani kwake na kumtaka alale na mdogo
wao wa kiume wakati huo akiwa na mwaka mmoja na binti akipitiwa na
usingizi humvua nguo za ndani na kumwingilia huku akimtaka kukaa kimya
na kuvumilia maumivu.
Mke wa mtuhumiwa huyo, ambaye amekuwa akizimia
mara kwa mara kutokana na kulia baada ya kubaini mchezo huo, alisema
aligundua watoto wake wanabakwa Ijumaa iliyopita baada ya mmoja wa
mabinti zake hao kumweleza kuwa baba yake alikuwa amembaka Machi 19,
mwaka huu.
Alisema kabla ya binti huyo kumweleza hivyo,
alimwomba asimpige kwani kuna kitu anataka amweleze, japo ni kibaya
lakini yeye amechoshwa na kimekuwa kikimuumiza kichwa.“Alisema kila ninapokwenda katika biashara zangu,
anatamani nisiwe ninawaacha hapo, nikamwahidi sitamfanya kitu ili mradi
aseme ukweli tu,” alisema mama huyo. Baada ya kuhakikishiwa kulindwa, ndipo binti huyo
aliposimulia jinsi ambavyo baba yake amekuwa akiwafanyia na kuwatishia
wakipiga kelele atawaua.
“Niliposikia mwili ulisisimka na ghafla binti
yangu mwingine naye akatokea akilia na kuniambia, ‘hata mimi baba
ananifanyiaga hivyohivyo kila siku unapokuwa umepeleka mboga sokoni
Kariakoo,” alisema mama huyo. Mwanamke huyo ameomba sheria ichukue nafasi yake
katika tukio hilo kwa kuwa ni la kinyama na pia wataalamu wa saikolojia
wamsaidie binti yake mdogo wa darasa la tano kwani yeye ameathirika
zaidi. Daktari aliyewapima watoto hao, ameshauri binti huyo mdogo apate ushauri zaidi ili kurudisha akili yake katika hali ya kawaida.
Simulizi za watoto
Wakizungumza nyumbani kwao jana watoto hao,
walisema baba yao alikuwa akiwatishia kuwakatakata kwa panga au kuwakaba
koo humohumo chumbani endapo wangethubutu kumweleza mtu yeyote kitendo
wanachokifanya.
“Tulikuwa tumeingia kwetu kulala na wadogo zangu,
nikasikia ananiita nikambembeleze mtoto eti anamsumbua, nilikwenda
nikambembeleza akalala, wakati nashuka kitandani kurudi chumbani kwetu
baba akanivuta kwake akanivua, akasema anachokifanya ni suna kwa hiyo
hataki kelele, akisikia atanikaba nife.”
“Niliumia sana na asubuhi mama alirudi
nikajitahidi kweli asijue na hata shule sikwenda, jioni mama aliondoka
tena baba hakuniita siku hiyo lakini baada ya siku tatu aliniita tena
ikawa vilevile navumilia. Siku zilivyozidi unaweza kukuta kwa wiki
naitwa hata mara nne siku ambazo mama hayupo nyumbani,” alisema.
Watoto hao walieleza kuwa baadaye baba huyo
alihamia kwa binti mdogo kwa staili ileile na kila mmoja alikuwa akiitwa
kwa zamu na kwa vile kila mmoja alijua ni siri yake na baba. Kutonaka
na woga wa kuuawa, hakuna aliyemweleza mwenzake hadi katikati ya mwaka
jana mmoja wao alipomweleza mwenzake na baadaye kumweleza mama yao.
“Baba alikuwa anasema atatuua bila hata mtu kujua
na tutaozea shambani, hata nikiwa katika siku zangu baba ananiingilia
hivyohivyo, naugua kila mara UTI, mdogo wangu naye kila mara UTI,
tukaamua liwalo na liwe kama kufa basi ila mama ajue,” alisema mtoto
huyo huku akibubujikwa na machozi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Miembe Saba,
Hamis Shomari alisema kabla ya kupelekwa kituo cha polisi Kongowe
Jumamosi iliyopita, watoto hao waliitwa shuleni hapo na kuhojiwa kila
mmoja peke yake na wote walikiri kuanza kubakwa mwaka 2013 na baba yao
na kwamba tabia hiyo iliendelea hadi Machi 19 usiku alipobakwa binti
mdogo kwa mara ya mwisho na Machi 20 walipoamua kumweleza mama yao.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei
alisema wanamshikilia mtuhumiwa huyo na kwamba wasichana hao wamefanyiwa
vipimo mbalimbali na majibu ya daktari yamethibitisha kuwa wamebakwa na
sehemu zao za siri zimeharibiwa, hivyo wanaendelea na matibabu.CHANZO MWANANCHI.
Maoni 2 :
Pole sana na hatua zichukuliwe. Jamani wanaume kuna wanawake wengi kwanini ubake wanao??
Kuharibika sijaelewa kwani muda ungekuwa mrefu wanafanya kite ndo waliingiliwa kinyume cha maumbile
Angepigwa ahanithiwe . Wanauwa Wizi hata wa simu kwa nini wamwache huyo looh Mungu tulindie watoto
Chapisha Maoni