Pages

Ijumaa, Aprili 24, 2015

Wataalamu wajitokeza kumsaidia Wema Sepetu (kufuatia suala la kutopata ujauzito)Kufuatia  tatizo la kushindwa kupata ujauzito alilonalo msanii maarufu Bongo, Wema Sepetu, hivi karibuni waganga wapatao 26 kutoka sehemu mbalimbali nchini walijitokeza na kuomba kuunganishwa na staa huyo ili wamtibu.

Waganga hao wa tiba asilia pamoja na madaktari kutoka hospitali mbalimbali kwa nyakati tofauti walipigia simu  na kueleza kuwa, wanashangaa kuona Wema anakosa amani wakati wao wanaweza kumtibu na kuweza kuitwa mama kama wenzake.
Unajua wapo wanawake ambao wanakosa amani kwa mambo ambayo hawastahili, hili la Wema kutopata mtoto linatibika, mpeni namba yangu kisha anitafute,” alisema mmoja wa wataalam hao aliyeomba jina lake lisiandikwe.

Katika kujua Wema anapokeaje ofa aliyopewa na waganga hao, alitafutwa na alipopatikana alikubali mara moja kutibiwa tatizo alilonalo lakini akatoa angalizo.

Kuna watu wengi sana ukiacha ambao wamejitokeza kwenu, mimi nina meseji zaidi ya 400 ambazo nimetumiwa kwenye namba yangu ya WhatsApp na simu kibao nimepigiwa watu wakijitolea kuja kushughulikia tatizo langu, kiukweli kabisa nipo tayari.

Lakini ni vizuri wakati naanza kutibiwa tayari nikawa na mwenza wangu ambaye tutakuwa tumekubaliana na pale tatizo litakapoisha, iwe rahisi kuzaa mara moja,” alisema Wema.CHANZO UDAKU SPECIAL

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom