Ijumaa, Mei 22, 2015

MAONI YA MDAU "UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU UWE WA AMANI"


Mwaka huu wa 2015 Watanzania tunatarajia kufanya uchaguzi wetu mkuu wa ngazi ya madiwani, wabunge na Rais. Ni kipindi kizuri kuwapima wagombea wote watakaojitokeza kuomba ridhaa  kwa mara nyingine sambamba na wagombea wapya. Tuwapime wagombea wote kwa hoja na sera zao , nao wenyewe na vyama vyao. 

Tutambue tukifanya kosa lolotee lile katika kufanya maamuzi haya nyeti,  litagharimu kwa miaka mitano ijayo, yaani hadi mwaka 2020. Wakati tunajipanga kwa uchaguzi huu mkuu tusisahau kudumisha amani ya nchi yetu. Vilevile tuhakikishe kuwa hatuendelezi rushwa  ili kweli tuweze kuwapata viongozi tunaowahitaji na wenye uwezo wa kuongoza.


 Imekuwa ikitokea kuwa baadhi ya watu baada ya kupewa pilau au doti ya kanga tu wanaweza kuburuzwa na mgombea ambaye hana uwezo zaidi na rushwa ndogo aliyotoa ambayo itawagharimu wananchi kwa miaka mitano ijayo, huku kukiwa hakuna njia ya kumn'goa mtu wa aina hiyo.Nadhani wote tutatumia nafasi yetu vizuri ili kura ya kila mmoja iweze kupata thamani yake. SUZANA MWANANGWA KUTOKA IRINGA

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom