“Tunawajibu mkubwa wakutambua kwamba umuhimu wa siku hii ni wakipekee ambapo kila Mdau iwe Serikali ,Taasisi, Jamii au hata mtu mmoja mmoja lazima aguswe na maadhimisho hayo kwa namna moja au nyingine hasa ikizingatiwa kwamba tatizo la Dawa za kulevya tayari limeshaigusa kila Familia katika Nchi yetu”,amesema Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Mhe. Fatma Abdulhabib Fereji amesema dawa za kulevya ni janga la Kidunia linalopigwa vita na Mataifa yote Duniani.
Madhara ya Dawa za Kulevya
Kuendelea kutumia Dawa za Kulevya husababisha utegemezi ambao humfanya mtumiaji apate madhara mbalimbali ya kiafya na hata vifo. Kwa ujumla madhara ya Dawa za Kulevya ni makubwa sana. Madhara ya Dawa za Kulevya kwa mfano Bangi, ni Makubwa kwa Watumiaji wenyewe, familia zao, Ndugu zao, Jamii wanamoishi na Taifa kwa ujumla. Starehe ndogo ya mwanzo na ya muda mfupi huleta adha kubwa na ya muda mrefu kwa jamii nzima. Ukubwa wa Tatizo
Kwa bahati mbaya, rika la Watumiaji wa Dawa hizi wengi ni Vijana ambao ndio rika linalotarajiwa kuzalisha na kutoa Viongozi wa baadaye. Aidha, watumiaji hawa ndio wazururaji, waporaji na wabakaji mitaani. Watumiaji hawa ndio ambao wanakuwa ombaomba mitaani na mwisho kukumbwa na magonjwa ya akili, UKIMWI na hatimaye vifo. Vilevile imebainika kwamba, Vijana wengi hapa Nchini wanajihusisha na matumizi ya Dawa za Kulevya.Kumbuka "IMARISHA AFYA EPUKA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni