Pages

Jumatano, Juni 24, 2015

SIMULIZI "NIMEKUCHOKA"


"Unajua ni muda mrefu sana tumekuwa katika mahusiano, takribani miaka saba sasa. Lakini mwenzangu kila nikikuambia suala la kufunga ndoa naona unanipiga danadana, unajua mimi nakupenda sana Fredy lakini nashindwa kuelewa kwanini inashindikana kukamilisha lengo la mahusiano yetu na tufunge pingu za maisha, tafadhali mpenzi wangu nakuomba uwe muwazi kwangu,  wakati mwingine mimi nafikiria kuwa labda umepata mwanamke mwingine  yaani sikuelewi hata kidogo".

 Alikuwa anazungumza Fatuma huku akimtizama Fredy ambaye alionekana kunyamaza kimya  kana kwamba alikuwa hasikii au hajaelewa kile alichokuwa anaelezwa. Fatuma aliendelea kuzungumza na kusema "Inamaana hunisikii ninachozungumza Fredy jamani" Fredy alimgeukia kisha akasema "Yaani wanawake mnamatatizo sana hivi kuna kitu gani ambacho unakikosa kutoka kwangu, kama mapenzi unayapata, mtoto tunaye, kila kitu nakuhudumia, na isitoshe tunaishi vizuri tu yaani mimi na wewe ni tayari mke na mume, sizani kama kuna haja ya kufunga ndoa.

 Halafu mbona umekuwa na kiherehere cha ndoa kiasi hicho, au unataka tu sherehe, watu waje wamevaa sare wacheze mziki halafu wale na kunywa sasa ndiyo itasaidia nini, mimi naona hizi habari za ndoa tuachane nazo kabisa" 

Aliongea Fredy kwa msisitizo na huku akionyesha kujiamini zaidi, wakati wote huo Fatuma alikuwa akimsikiliza kwa umakini, alimtizama kisha aliguna kidogo na kusema "Inamaana Fredy leo hii unaniona mimi nina kiherehere cha ndoa, siamini kwakweli hivi unakumbuka ahadi ulizonipa kuhusu maisha yetu, kwanza nilipata ujauzito wakati nikiwa nipo chuo nasoma na wazazi wangu walikuwa wakali sana kwangu, lakini nilivumilia nikijua kuwa ipo siku utakuja kujitambulisha nyumbani, na kipindi chote cha ujauzito ulikata mawasiliano kabisa, yaani hukuniudumia hata kidogo ijapokuwa ulikuwa unafahamu kuwa mimi sina kazi.

Nilimuomba sana Mungu anisaidie niweze kuvuka safari ile salama, na kweli ilifikia kipindi nikajifungua salama na wazazi wangu ndiyo walionilea kwa kipindi chote hicho hukuonekana, baada ya mwaka mmoja ulirudi na kuniomba msamaha ukinitaka nifungue moyo wangu ili tuweze kumlea mtoto wetu Ritha pamoja.

Ijapokuwa  ulinitelekeza kipindi cha ujauzito, lakini bado moyo wangu ulikuwa unakupenda, yaani sikusita kukusamehe Fredy, ndugu na marafiki zangu walinishangaa na kunicheka sana kwanini nimeamua kukusamehe lakini nilijaribu kukutetea nakusema kuwa umejutia makosa yote uliyonitendea.

 Tena nilipokusamehe baada ya muda ukawaeleza wazazi wangu kuwa unataka kunioa, yaani tokea ulipotoa mahari nyumbani kwa wazazi wangu ni miaka mitatu sasa imepita, hivi kweli Fredy inamaana yote hayo hukumbuki leo hii unaniona mimi nina kiherehere na ndoa, nimekuvumilia sana mpenzi wangu embu fikiria hapa tulipo tunaishi mikoa tofauti mimi nafanya kazi Arusha na wewe unaishi Mwanza halafu kuonana kwetu mimi na wewe wakati  mwingine inapita takribani miezi sita.

 Hivi unafikiri kama tungekuwa tumefunga ndoa ni lazima  tungejua muafaka wa nini tufanye ili tuweze kuishi sehemu moja, ila mwenzangu unalichukulia hili jambo kama la kawaida inaniuma sana yaani sana” Aliongea Fatuma kwa uchungu sana huku machozi yakiwa yanamlengalenga, Fredy alimtizama kisha akacheka kicheko cha kebehi nakusema .

“Kwahiyo unanieleza hayo yote ili mimi nikusaidieje, inamaana hivyo unavyozungumza unalalamika, au unalazimisha ndoa? Ngoja nikuambie kitu kimoja Mama Ritha mimi sina mpango wa kuoa kwasasa, kama nilivyokueleza haya maisha tunayoishi mimi naona ni sawa hayana tatizo na pia labda yawezekana kuna mwanaume mwingine amekuambia kuwa anataka kukuoa basi nenda kaolewe, usitake kunipigia makelele tena sihitaji kuendelea na mazungumzo nataka nipumzike” 

Aliongea Fredy huku akimtizama Fatuma kwa kumkazia macho Fatuma alisimama nakusema “Asante sana Fredy, kwa majibu yako ama kweli maji yamenifika shingoni, ukweli ni kwamba nimekuchoka, yaani mimi nimebadili dini yangu na kukufuata wewe ili tuweze kuishi pamoja leo hii unanidharau sawa, ila nimechoka na sasa ni bora nikuache na wewe uwe huru, umesema niolewe kama nataka kuolewa sawa mimi bado ni mwanamke mrembo Mungu atanijalia nitampata ambaye ni chaguo langu asante sana. JE UNATAKA KUJUA NINI KILIENDELEA ANDIKA NDIYO ILI NIKULETEE MWISHO WA SIMULIZI HII

Maoni 7 :

Bila jina alisema ...

NDIYO!!!!! Hii hadithi tamu dia!!!! Nasubiria sehemu ya pili.

zuwena alisema ...

ndiyo nijue mwisho wa huyo dada

Bila jina alisema ...

ndiyo

Bila jina alisema ...

Ndio ni hadithi nzuri na ina mafunzo

Bila jina alisema ...

ndiyo Adela hadithi nzuri

Unknown alisema ...

Ndio

Alima Ndarurinze alisema ...

Ndio

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom