Jumanne, Juni 23, 2015

"macho yanaweza kudanganya lakini moyo unasema ukweli"

Ni vigumu sana kutambua ukweli kwa kumtizama mtu machoni, kwani yawezekana kile anachokisema siyo ambacho kipo moyoni mwake, ukweli ama uongo anaozungumza mtu  wakati mwingine yeye ndiye anayejua moyoni mwake kile alichomaanisha. Mfano katika mahusiano mtu anaweza kusema anakupenda sana kuliko kitu chochote, lakini vitendo vyake vikakuonyesha je ni kweli amemaanisha kutoka moyoni, na vitendo vyake hivyohivyo vinaweza kuonyesha uongo au ukweli wa alichokisema.
 Pia katika uchaguzi Mkuu ujao ni muhimu sana tukawa makini kwani siyo kila kiongozi anayesema atatusaidia wananchi katika mambo mbalimbali basi atatenda hivyo, kwani wapo wanaotamani kuwa viongozi kwa manufaa yao binafsi. Maisha hayatabiriki ni muhimu kuwa makini kwa jambo lolote linalotuzunguka.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom