Pages

Alhamisi, Julai 02, 2015

"Aliyetenda makosa anaweza kuwa bora zaidi kuliko yule ambaye hajawahi kutenda makosa"

Ukweli ni kwamba hakuna binadamu aliyekamilika kwamba kila atakachokifanya katika maisha yake kitakuwa sawa bila kufanya makosa, lakini pia ni wachache sana ambao hawajawahi kufanya makosa na sikuzote kama wewe ni mtafutaji hutakiwi kuogopa kufanya makosa bali unachotakiwa kufanya ni kutambua makosa uliyofanya na kuwa makini usirudie kufanya makosa,.

Mara nyingi tunajifunza kulingana na makosa yaliyotokea katika maisha yetu, ila ni mbaya sana kama utakuwa unatenda makosa halafu haujifunzi yaani kila siku unarudia makosa. jambo la msingi katika safari ya mafanikio usiogope kusonga mbele, kwani unaweza kuwaza kuwa utashinda au utashindwa lakini tu usikate tamaa na endelea kusonga mbele.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom