Pages

Jumapili, Julai 12, 2015

HAYA NI MACHACHE ALIYOSEMA MHESHIMIWA RAIS DR. JAKAYA KIKWETE WAKATI AKIFUNGA MKUTANO MAALUMU WA CCM MWAKA 2015.

"Wale waliozani CCM ingesambaritikia hapa wameula wa chuya". Ilani imetekelezwa vizuri sana mengi yamekamilika na yale ambayo hayajakamilika yapo kwenye utendaji, ilani iliyotayarishwa ni nzuri imezingatia wakati tulionao na ujao imeweka mikakati ya yaliyofanyika na yaliyofanikiwa na pia imetoa maelekezo mapya katika serikali mbili ya nini kifanyike.

Ilani inayo maono ya mbali yenye uthubutu, kuwa na ilani ni namba moja lakini namba mbili ni kuwa na wagombea wazuri watakao inadi ilani hiyo, nakupongeza Magufuli kwa kuchaguliwa kwa kura nyingi sana wamekupa imani kubwa ambayo unaistahili na siyo ya kubahatisha, kwanza umethibitisha kuwa kuwa una moyo wa kuona jambo linatendeka na ni msukumaji kweli wa mambo tingatinga, na wale waliozoea kuishi kwa rushwa za kupata viwanja walipata shida sana na waliokuwa wanafanya uvuvi haramu walipata tabu sana alikuwa anafanya jambo lenye msaada kwa wewe mwenyewe mvuvi.

Kwenye upande wa barabara umefanya kazi kubwa sana na Magufuli ni mbunifu sana yaani ni jembe tena zaidi ya jembe mimi naamini kwa sifa ulizozijengea ukiwa Rais wa nchi yetu Tanzania itanufaika sana, halafu ndugu Magufuli pia avumilii ujinga, watanzania mpate nini tena, mimi nakuamini Magufuli kasi iongezeke tupunguze umasikini.

lakini hata na wewe unahitaji mtu wa kukusaidia Samia Hassan ni waziri wangu anashughulikia masuala ya Muungano na tutaingia katika historia nchi yetu kupata makamu wa kwanza Rais mwanamke, nawatakia kila la heri kunadi ilani ya chama cha mapinduzi kazi ambayo ni yetu sote, pia nawapongeza Dr Migiro na Balozi Amina kwa kujitokeza na kufikia hatua ambayo siyo jambo dogo na pia ni uthibitisho kuwa wanawake ukiwapa fursa wanaweza.

Sasa kazi yetu ni kusaka ushindi wa ccm temu Magufuli imeshaondoka sasa ni timu ccm.Namnukuu Rais Jakaya Kikwete kutoka Mkutano Mkuu Maalum wa CCM 2015.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom