Pages

Jumapili, Julai 12, 2015

HAYA NI MACHACHE ALIYOSEMA MGOMBEA URAIS KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI DR.JOHN MAGUFULI BAADA YA KUIBUKA KIDEDEA.

Mgombea Urais chama cha Mapinduzi, Mheshimiwa Magufuli kutoka Mkutano Mkuu Maalum wa CCM amesema, Namshukuru mwenyezi Mungu pamoja na wajumbe wote,nashukuru mmekubali kunituma tena kwa kura za kishindo asanteni sana tena sana mmenipa heshima kubwa naahidi kuzinadi sera za chama cha mapinduzi kazi hiyo nitafanya na ninyi ili tupate ushindi mkubwa na wa mafanikio, wingi wa kura hizi ni uthibitisho kwamba ccm ipo juu.
kinachotakiwa ni umoja na ushikamano wetu tuungane wote kuhakikisha chama chetu kinapata ushindi mkubwa sana, chama ambacho kina misingi imara ya kupata viongozi,chama kilichokomaa mtandao wetu wa ushindi ni mmoja yaani ccm nitafanya kila jitihadi kuzilinda ilani za ccm nawashukuru sana wote nawathibitishia nitakuwa mtumishi wenu.nimeamua kumteua mgombea mwenza awe Samia Suluhu Hassan.

Mgombea mwenza Samia Suluhu Hassan ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano. 

Dr Asha Migiro amesema, Nachukua fursa hii kuwapongeza wanawake wenzangu waliochukua fomu ya kugombea Urais pamoja na wana ccm wote Rais anaweza kutoka chama chochote lakini Rais bora atatoka ccm akimnukuu Mwalimu Nyerere pongezi za dhati kwa mheshimiwa John Magufuli na mama Janeth Magufuli pamoja na Balozi Amina Alli.
Kura alizopata mheshimiwa Magufuli ndiyo sahihi kabisa na ndiyo siri ya ushindi wetu, tumeonyesha kuwa tuko tayari kushinda ninaahidi kuwa nitaungana na wana ccm wenzangu kuhakikisha mheshimiwa John Magufuli anapeperusha bendera ya ccm mimi na mwenzangu mhemishiwa Amina tumeonyesha uthubutu hivyo vijana wa kike watambue kuwa tunaweza na tunaweza sana.
Balozi Amina amesema nachukua fursa hii kuwashukuru wote, kwani  heshima niliyopewa ni heshima kubwa nitaendelea kuwa mtiifu katika chama chetu cha Mapinduzi, nawahakikishia  kuwa nitamuunga mkono mwenzetu ndugu John Magufuli ili chama chetu kipate ushindi wa hali ya juu,nawatoa hofu wanachama akinamama kuwa ndani ya ccm kuna utajiri kwa kina mama wenye uthubutu.
Chama cha mapinduzi kimeandika historia wanawake tunaweza tupeleke majeshi yetu kwa mheshimiwa Magufuli ili tuongeze ushindani mimi nipo mstari wa mbele kabisa kushirikiana na Magufuli tukumbuke chama kwanza na siyo mtu, nakuombeni ndugu zangu majeshi yetu yote tuyapeleke kumuunga mkono mheshimiwa Magufuli ili chama chetu kipate ushindi wa hali ya juu.


Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom