Pages

Jumapili, Julai 12, 2015

HAYA NI MACHACHE WALIYOZUNGUMZA WAGOMBEA WATATU KUOMBA KURA ZA WAJUMBE KUTOKA MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM 2015Nina Miaka 38 ndani ya chama na miaka 42 ya kiutendaji mimi sina adui wala sina kundi hivyo nitaunganisha makundi yote tuwe kitu kimoja, mimi nitadumisha muungano kwa kila hali.wakati ni leo kuthibitisha wanawake wanaweza naomba nipate ridhaa ya kufanya kazi na mheshimiwa Lowasa. Amesema  Balozi Amina Salim kutoka mkutano mkuu maalum wa ccm 2015

Endapo nitapata fursa hii nitasimamia umoja wa taifa letu nitadumisha muungano na pia nitaongozwa na ilani ya mapinduzi ili kuhakikisha tunasonga katika nyanja mbambali za maendeleo.Amesema Asha Rose Migiro kutoka Mkutano Mkuu maalum wa ccm 2015

Chama kimenilea hadi kufika hapa, naomba kura kwasababu naamini nitafanya kazi na ninyi pia naamini nitakilinda chama chetu cha mapinduzi ili kiendelee kushinda pia ninaamini nitaulinda muungano wetu napenda kuahidi kuwa sintowaangusha, nimefanya kazi na mheshimiwa Kikwete miaka kumi naamini sikumuangusha nataka niwathibitishie nitafanya kazi nanyi bega kwa bega hata ninapozungumza wapinzani matumbo joto naamini sintowaangusha ninawaomba sana mnitume hii kazi ya kukiwakilisha chama changu katika kuleta maendeleo.Amesema John Pombe Magufuli kutoka mkutano mkuu maalum wa ccm 2015.

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom