Dk. Magufuli alisema endapo atachaguliwa kuwa Rais wa,
atashirikiana na vyama vingine vya siasa kwa lengo la kuharakisha
maendeleo ya Watanzania.
“Umoja wetu ambao umeasisiswa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi
tangu enzi za Uhuru ni lazima Watanzania na wana-CCM waendelee kuulinda
kwa nguvu zote,” alisema Dk. Magufuli.
Alisema atahakikisha anasimamia vyema ilani ya uchaguzi ya CCM ili
kuleta maendeleo katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kimaendeleo
ambayo ndiyo nguzo kuu ya kuwakomboa Watanzania.
“Ilani ya Chama cha Mapinduzi imezungumzia mambo kibao,
tutahakikisha sisi wote wagombea watatu wa CCM na viongozi wengine wa
chama tunashikamana kwa pamoja katika kuitetea Ilani ya uchaguzi ya
CCM,” alisema.
Alisema endapo atapata ridhaa ya Watanzania na kushinda
atahakikisha anashirikiana na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein kwani kiongozi huyo ni muadilifu na asiyekuwa na majivuno.
“Dk. Shein hana majivuno, hana makuu, anampenda Mungu na anawapenda
Wazanzibari na Watanzania wote, napenda kuwaahidi wote na hata wasio
wana- CCM kwamba nitatoa ushirikiano kwa Dk. Shein ili kuleta
maendeleo,” alisema Dk. Magufuli.
Naye Mgombea mwenza kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan, alisema
uteuzi huo umedhihirisha wazi kuwa chama hicho kimeweka historia kwa
kumteua mwanamke katika ngazi ya juu ya uongozi.
Alisema hayo jana baada ya kupokelewa katika viwanja vya ndege vya Abeid Karume
Zanzibar na na umati mkubwa wa wananchi na wanachama wa
chama hicho.Katika mapokezi hayo, Magufuli alisindikizwa kwa msafara wa pikipiki na
magari huku wafuasi wa chama hicho wakiwa wamevaa sare zenye rangi ya
njano na kijani. moja kwa moja katika makao makuu ya CCM
Kisiwandui na kuzuru kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid
Amani Karume kisha kuzungumza na wanachama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni