Kiongozi mkongwe wa chama cha mapinduzi (CCM) Mzee Kingunge Ngombale Mwilu akizungumza na vyombo vya habari nyumbani kwake jijini Dar es salaam nakusema mchakato wa kumpata mgombea Urais kupitia chama hicho ulikuwa batili kutokana na kamati ya maadili ambacho ni chombo cha ushauri, Kufanya kazi ya Kamati Kuu ambayo ni kutoa maamuzi.
Amesema kamati ya maadili ilivunja maadili lakini pia aliongeza katika hilo inaonyesha kuna watu walikuwa na orodha yao kuhusu nafasi ya Urais pia, amemzungumzia Waziri mstaafu Mheshimiwa Edward Lowasa kuwa hausiki kwenye kashfa yoyote ya ufisadi kwa maana yeye aliwajibika kisiasa, na siyo kwamba alihusika katika kashfa ya Richmond vilevile Kingunge ametoa angalizo kwa viongozi wa ngazi ya juu wa Chama Tawala.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni