Pages

Jumapili, Novemba 22, 2015

WAOGOPE SANA WATU BANDIA KATIKA MAPENZI


Safari ya mapenzi inachangamoto nyingi sana, unaweza kukutana na mtu ukaamini kuwa huyu ananipenda na kamwe hatonitenda lakini ikawa sivyo unavyofikiria, unaweza kupenda kwa moyo wako wote lakini mwisho wasiku ukaambulia maumivu bila penzi la kweli.

 Kuna baadhi ya watu ni bandia katika mapenzi, watu hawa hujifanya wanapenda lakini kumbe si kweli, utakuta mtu anakubembeleza  kwa maneno mazuri kama "Nakupenda sana mpenzi wangu kamwe siwezi kukuacha wewe ndiye chaguo langu" Na maneno mengine mazuri zaidi ya hayo lakini baada ya muda anabadilika na kusahau ahadi zote mlizopanga pamoja, inaumiza sana, pale unapompenda mtu halafu akakufanyia mambo ya ajabu.

 Wakati mwingine ni vigumu kumtambua mpenzi wa kweli katika maisha, kwani yule unayemfikiria anaweza kuwa siyo sahihi kwako, na yule ambaye hukuwahi kumfikiria akawa ndiyo chaguo sahihi katika maisha yako, jambo la msingi ni kumshirikisha Mungu akusaidie ukutane na mtu sahihi katika maisha yako.

 Kuna vitu vingi vinapelekea kukata tamaa  ya kupenda tena moja ikiwa ni kupitia changamoto nyingi katika mahusiano, na kufikia kipindi kusema kuwa siwezi kupenda tena, kwasababu haukuwahi kupata furaha ya mapenzi siku zote kwako mapenzi yamekuwa ni karaha.

Je unafikiri nini kifanyike pale unapoona mapenzi kwako ni maumivu kila siku, baadhi ya wanasaikolojia wa mapenzi wanasema "Ni muhimu kuwa makini unapotoka katika maumivu ya mapenzi ili usijikute unaingia kwenye mahusiano mengine ambayo utapata maumivu makali zaidi ya mwanzo. Kwani baadhi ya watu wamekuwa wakichukulia matatizo ya mapenzi yaliyopo kwa muhusika na kujifanya kuona  huruma. Halafu mwisho wa siku unajikuta ukifikiri huyo anayekuonea huruma anakupenda kumbe na yeye akishakupata atakutenda na kujikuta unapata maumivu maradufu".

 Kwahiyo ni vyema kuwa makini sana, usikurupuke kuanzisha uhusiano mpya bila kukaa na kutafakari kwanini mwanzo ilishindikana,  Mapenzi ni matamu sana ukimpata anayejua kupenda na mapenzi ni machungu sana ukikutana na asiyejua nini thamani ya penzi la kweli. Imeandaliwa na Adela D. Kavishe

Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom