Pages

Ijumaa, Januari 08, 2016

"MAPENZI KAMA AJIRA"


Mapenzi kama ajira wapendwa wangu wakati mwingine huwa siwaelewi watu wanaoyaponda mapenzi maana kila mwanadamu anahitaji upendo kuna stage ambayo wazazi wako watakuonyesha mapenzi ya hali ya juu ukiwa nao, Utabembelezwa, utapikiwa chakula, utalishwa, Utaogeshwa, utaambiwa maneno mazuri na matam, na ikishapita hiyo stage Mapenzi hayo hayo utayapata kwa mpenzi wako, mkeo au mumeo. 
So unapoingia kwenye mahusiano ya mapenzi jua umeingia kwenye Ajira ni lazima ujue kumlea mwenzio kwa kumbembeleza, kwa maneno mazuri na ya kutia moyo,ujue kucheza na ufahamu wake pamoja na akili yake,ili utambue nini na kipi anahitaji na kwa wakati gani, kama ambavyo ulivyo makini kwenye kazi za boss wako au biashara zako ndivyo hivyo ambavyo unapaswa kuwa kwa mwenza wako, maana Dunia hii imebebwa na mapenzi.
 Ukiharibu kwenye mapenzi kamwe huwezi kufanya vizuzi kwenye biashara zako na huwezi kufanya vizuri kwenye Ajira yako maana moyo na akili yako vikivurugwa hata mwili hudhoofika, Nawapenda sana nawatakia siku njema na Baraka tele kwenu pamoja na wapenzi wenu mmwah! mmwah! Ujumbe huu umeandikwa na Ester Charles kutokaukurasa wake facebook.


Hakuna maoni:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom