Pages

Ijumaa, Januari 15, 2016

SIFA KUU AMBAZO WANAUME WENGI WANAZIPENDA KUTOKA KWA MWANAMKE


Hizi ni sifa kuu ambazo wanaume wengi wanazipenda kutoka kwa mwanamke 
 (1) mwanamke mtii. Kila mwanaume ana vitu vyake ambavyo hupenda mwanamke wake avifanye au aviache so mara nyingi mwanaume hufurahia utii kwa mwanamke wake (lakini tii kwa mambo ya msingi ambayo hayamchukizi MUNGU ).

(2) Mwanamke msafi. Kila mwanaume anapenda kuwa na mwanamke msafi anaejipenda yeye mwenyewe na anaependa mazingira yake na mumewe na mtoto watoto wake.


 (3) Mwanamke mwenye hofu ya MUNGU. Mwanamke mwenye hofu ya MUNGU huwa sambamba na mwanaume wake kwa kila jambo, lakini asiyekuwa na hofu na MUNGU hawezi kuwa mtii wala msikivu kwa mwanadamu mwenzie.

 (4)Mwanamke anaejipenda na kujua thamani ya utu wake. Mwanamke anaejipenda nafsi yake na kutambua thamani yake hawezi kusahau thamani ya mwanaume wake maana kaishajijua yeye thamani yake na utu wake hivyo ni rahisi kutambua thamani na utu wa mwanaume wake. 

(5)Mwanamke mkweli. Mwanamke mkweli na muwazi hupendwa na jamii yote inayomzunguka.

 (6) Mwanamke mpenda maendeleo. Mwanamke mpenda maendeleo ni fahari ya mwanaume yeyote maana mwanamke anaweza kuleta mafanikio makubwa sana kwa mwanaume kupitia akili yake ya kupenda maendeleo.

 (7) Mvumilivu. Mwanamke mvumilivu ni faraja kwa mwanaume wake maana hata mwanaume akiyumba kiuchumi hatamkimbia na wala hatachepuka Bali atampa moyo na faraja ambayo itamfanya mwanaume huyo aendelee kukaza buti. 

 (8)Mwaminifu kwenye mahusiano. Kila mwanaume anapenda awe na mwanamke wa kwake yeye mwenyewe , yaani mwanaume hata awe kicheche vp anapenda kuwa na mwanamke mtulivu.

 (9) Mwanamke mchapakazi. Wanaume wengi wanapenda mwanamke mwenye adress yaani awe na sehemu ya kumuingizia hata hela ya wanja siyo aombe kila kitu.

 (10)Mwanamke anaejituma kumfurahisha mwanaume wake kwenye 6×7 . Kila mwanaume anapenda kupata kitu kizuri na cha tofauti kutoka kwa mwanamke wake so kila mwanamke anapaswa kutumia akili yake yote na nguvu zake zote kwenye huo upande, acheni uvivu wadungu HAPO KAZI TU. nawatakia siku njema nawapenda san. Imeandikwa na Esther Charles  kupitia ukurasa wake wa instargram.

Maoni 2 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Adela Ahsante kwa kwa kutokuwa mchoyo...nimepenza hizi sifa nadhani hutajali kama nikiwema pale kibarazanikwetu pia...

Adela Kavishe alisema ...

pamoja sana Yasinta bila shaka.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom