Jumanne, Desemba 21, 2010

Lainisha Uso wako kwa kutumia nyanya na asali...kwani vipodozi vya asili ni bora zaidi.

Watu wengi wanadhani kutumia vipodozi vya asili ni urembo wenye mchakato mrefu na mgumu lakini kama unaipenda ngozi yako naamini hautaona ugumu wa kuitunza kwa vipodozi vya asili.Jinsi ya kulainisha uso kwa nyanya na asali.Chukua nyanya moja kubwa iliyoiva kisha imenye na kuisaga na uji wake paka usoni ukimaliza chukua asali mbichi kisha changanya usoni na nyanya baada ya hapo acha kwa robo saa hadi ikauke kisha nenda kaoge.Kausha uso vizuri na taulo safi na rudia hivyo mara mbili kwa wiki na utapata matokeo mazuri kwa ngozi ya uso ,na njia hii inawafaa zaidi wenye chunusi ,kwani huwasaidia katika matatizo kama hayo.


Vipodozi vya asili navipenda sana kwani kwa ujumla havina gharama na vinanisaidia kuitunza ngozi yangu na kuiweka afya yangu salama tumia sasa nauone faida zake.


Maoni 6 :

Yasinta Ngonyani alisema ...

Adela! ahsante sana kwani hata mie huwa napenda vitu vya asili kama hivi. Ngoja nijaribu Lakini umesema asali mbichi ukiwa na maana gani?

ADELA KAVISHE alisema ...

@Yasinta tuko pamoja kipenzi asali mbichi ni ile itokanayo na nyuki wachanga ni nzuri sana na husaidia katika mambo mengi.

emuthree alisema ...

Kweli kumbe haina haja kukimbilia madukani kununua mavipodozi yaliyowekwa makemikali...umesaidia wengi Adela

Bila jina alisema ...

asante sana my dear, be blessed...

SophiesClub alisema ...

Ni kweli kabisa,vipodozi asili ni bora na matokeo yake ni mazuri.Asante sana

Unknown alisema ...

mmh! csta Adela ila ukipita mtaan utakuta asali nyingi tu zinauzwa, sasa utaijuaje ipi ni mbichi?, naomba msaada wako tafadhali.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...

share bottom